Jumapili, 3 Novemba 2013

WIMBI LA NGONO KATIKA JAMII NINI TATIZO?



ONGEZEKO LA WIMBI LA NGONO KATIKA JAMII YETU NINI TATIZO?

Hili tatizo sio nchini kwetutu bali limetapakaa ulimwenguni mwote ila kila sehemu kwa namna yake athari zake hazifanani wala vyanzo havifanani.

Kama ni mtanzania ambaye unaipenda nchi yako na unaifwatilia katika majanga mbalimbali ambayo nchi yetu inakumbwa katika kipidi hiki tulichonacho moja wapo ni uongezeko la vitendo vya ngono katika jamii tuliyo nayo na matokeo yake kusababisha madhara mbalimbali.

Ongezeko hili ni hatari kwa kuwa alina matokeo mazuri katika jamii tuliyo nayo katika Nyanja zote kijamii,kiuchumi na hata kisiasa zaidi sana kuchochea maendeleo kushuka katika jamii husika.

Japo wako watu wanafaidika kutokana na jambo hili hivyo mawazoni mwao ni kwa jinsi gani kuhakikisha jambo hili litazidi kukua na kukubalika katika jamii yote kwa ujumla.

Hivyo kuna mashindano ndani ya jamii moja wako watu ambao wanapenda jambo hili liendelee na wako watu ambao wanapenda jambo hili likomeshwe, pamoja hayo jambo hili alijahusisha watu wenye hali ngumu ya uchumi tu bali pia na hata watu ambao hawajui maana ya njaa au shida hivyo sio jambo utalifikiria kwa muda tu alafu ukalipatia utatuzi wa kudumu.

Jambo hili kwa watu wanaoshiriki wanaona wako sawa kutokana na sababu mbalimbali watakazo kukueleza na wengi wao wakisema hali mbaya/ngumu ya uchumi katika maisha.

Lakini ikiwa mtu ambaye unajielewa na kujithamini zaidi sana wazazi wenye akili nzuri na watoto wao hawafurahii jambo hili linapotendeka hasa likiwahusisha watoto wao au watu ambao wanao wapenda.
Ngono hivi sasa katika jamii yetu limekuwa ni jambo ambalo lisilo na heshima lilowazi ambalo akuna mficho tena katika jambo hili.

Hivi sasa unaweza kuamua leo kufanya ngono muda wowote na wakati mwingine kwa mtu unaye mtambua ambaye yuko tayari au kwa mtu ambaye umtambui lakini vilevile naye lazima awe tayari.

Kwa jamii tuliyo nayo sasa jambo ngono alina rika maalumu kwamaana sasa hata wanafunzi wa shule za msingi wanafahamu vizuri zaidi sana nao wanashiriki kuhusika na jambo hili au mahali maalum ila ni popote ambapo mtakubaliana au mmoja atapenda kushiriki swala hilo.

Katika jamii wako watu watu waliingia kutokana na msukumo mbalimbali baadae wakajuta na hata kujaribu kuhusia kwa watu wengine wasije kujiingiza katika hii biashara haramu lakini matokeo yake jambo hili linazidi kushika hatam siku baada ya siku.

Jambo hili limekuwa na sura yakutisha sasa ambayo imeota sugu, kama mti basi mizizi yake imekwenda mbali sana ambao ili kung’oa sio swala la mchezo tu.

Jambo hili limeleta matatizo katika jamii pindi linapozidi kuongezeka basin a athari zake zimekuwa zikishamiri kwa kiasi kikubwa;
i.kifo

wako watu kutokana na kutendwa na wenzi wao iepelekea kufa, kwa sababu kukosa kujua nini cha kufanya, japo hakuna mtu anaweza kuona nijambo lililo gumu sana mpaka kufikia hatua hiyo ya kujiua lakini limeshatokea katika jamii na bado linaendelea kutokea.

Japo unaweza kusema kifo ni mpango wa Mungu lakini jambo hili limekuwa likileta utata katika jamii yetu kwa kupoteza watu ambao tulio wapenda wanaweza kuwa wazazi,rafiki,ndugu wakaribu sana hata wako watu ulio wapenda na kuwaheshimu na kuwa thamini lakini kifo kimewatenganisha pasipo kutimiza yaliyo malengo yenu.
ii.kupoteza thamani ya ndoa

ndoa watu wakiishi kwa kujiami na kwa hofu kuu na sio kwakuona fahari ya kuwa huyu ni wangu na huyu si wa watu wengine. Watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa na mawazo mengi kuona tutadumu kweli je!tutafurahia ndoa yetu je! Moyo wangu hautajeruhiwa je! Maisha haya hayatanithiri kwa magonjwa.(shinikizo la damu,magonjwa ya ngono mfano.kaswende)

Waku hawana imani na wenzi wao pindi wanapo kwenda kazini,mashuleni na hata anapo pewa safari ya kikazi mashaka yanatawala maisha yake.

Neno kuwa niko tayari kuolewa au niko tayari kukuoa limekuwa likipokelewa kwa furaha lakini baadae uja na kuona ili neno lina maanisha kama linavyo tamkwa.

Hata walio katika ndoa wako watu wanafanya ngono na wasio wenza wao wengine wanafanya ndani ya nyumba na wengine mbali na makazi ya mwenzi wao.

Japo katika ndoa kuna sababu mbalimbali zinazopelekea hali kama hii lakini mwisho wa siku kunakuwa hakuna heshima katika ndoa na watu wengine hawataiheshimu kwa sababu ninyi wenyewe hamuipi heshima inayotakiwa.
iii.magonjwa ya zinaa

wako watu katika jamii yetu wanawalaumu wenzi wao kwa magonjwa waliyo yapata na kupelekea mateso ambayo wanaishi nao.

Kutokana na magonjwa haya ya ngono yanaathari mbalimbali mathalani kifo,kupunguza ufanisi katika kazi na hata kupelekea msongo wa mawazo, haya mambo haya yana sababishwa sana na wenzi wasio waaminifu lakini athari zake upelekea kwa wote wanaomzunguka.

Kuna mfano ambao niliosimuliwa na moja wa athirika hao katika ndoa:
Mama mmoja yeye aliye jitunza na kuthamini ndoa yake katika hali zote alidhamilia kuiheshim ndoa yake na kumjali mume wake kwa namna yoyote, siku moja mume wake alikuwa katika shughuli zake za kawaida kwakua alikuwa dereva wa magari ya mizigo akisafirisha mizigo kutoka sehemu mmoja na kwenda sehemu nyingine na hata wakati mwingine ilikuwa kutoka nchi moja na kwenda sehemu nyingine. Siku si nyingi mwanamke akapatwa na maradhi katika mwili wake na pindi alipoenda hospitalini kupata matibabu zaidi alijikuta ameathirika na virusi vya ukimwi na ndipo dhamira yake ikaanza kuyachunguza maisha yake na mwisho ukabani ni mume wake atakuwa amehusika ndipo walipokwenda nyumbani na kufanya majadiliano na mwenzi wake ndipo mwanaume alipogundua alishawai shiriki na wanawake wengi katika katika kufanya mapenzi na kukiri kuwa ugonjwa huo ameuleta yeye nyumbani sawa na dhamira yake ilivyokuwa ikimshuhudia.

Mwanamke huyu katika maisha yake alikuwa akimlaumu mume wake siku zote.

Hili nijambo ambalo lilikuwa ni fundisho kwangu na machozi ya Yule yalikuwa ni maneno yakisema ndani ya moyo wangu.
iv.moyo kujeruhiwa

hii ni kawaida kwa mtu aliyeshiriki tendo la ndoa na wewe kwa raha na huku wote mkifurahia ghafla ukakuta kunaanza kuwatofauti na vile mwanzo mlivyo kuwa inaweza kuwa katika muda kuwa mfupi katika kufanya tendo hilo au siku za kufanya tendo hilo kupunguwa kama mtu mwenye akili timamu kutakuwa na maswali mengi ambayo utakayo ukijiuliza kwa nini hali kama hii, bila shaka utaanza kujichunguza na kutaka kujua mapungufu ni yapi au nini umemboa au ulicho muuzi na pindi unapokosa jibu  moyo wako unakuwa nyong’onyea.

Na hali hii inapoendelea ndivyo moyo wako unazidi kujeruhiwa hatiamae kufikia kipindi kufanya yale ambayo hapo mwanzo ukuyafikiria kuyafanya.

Kidonda ndani ya moyo wako kuja kupona sio jambo la kawaida kinahitaji uwazi uliokuwa wa kweli ilikiweze kupona.

Moyo uliovunjika matokeo yake ni shinikizo la moyo,vidonda vya tumbo na maradhi ya mifupa pamoja na mengine mengi.
v.watoto wa mitaani

katika swala zima la ngono watoto wengi wanazaliwa katika maeneo yasiyo rasmi upelekea kukataliwa na hatimae kujitafutia maisha yao binafsi katika kudhi mahitaji yao.

Hakuna mtu anapenda haya matokeo lakini katika tendo hili watoto wanamna hii uweza kutokea na hatimae kupelekea ongezeko la watoto wamitaani, japo si wasemi vibaya watoto hawa wengine wasio na maadili upelekea unyang’anyi na upolaji katika mitaa.

Japo sio hawa tu wanafanya vitendo hivi ni watoto wa mitaani bali hata watoto wasio wa mitaani nao wameshiriki katika vitendo hivi vya uporaji na unyang’anyi.

Pamoja zipo athari nyingi zinazotokana na ongezeko hilo la ngono ndani ya familia,jamii na katika nchi kwa ujumla wake.

Tuone nini tatizo hatimae kupelekea uongezeko hili kuongezeka kwa kasi tena katika namna mbalimbali kwa uwazi mkubwa.
UTU KUKOSA THAMANI

Kwa upande wangu ninaona tatizo hili la ngono kuongezeka ni kukosa kuthamani utu wako binafsi japo kuna sababu mbalimbali kila mtu ukimuuliza kwa nini umeamua kushiriki mtandao huu wa ngono wengi watasema hali ngumu ya maisha,kusalitiwa na wenzi wao na nyingine nyingi.

Lakini mimi naomba nijikite katika hili watu kukosa kuthamini utu wao binafsi upelekea watu kuto kukuthaminiwa.

Unaweza kuwa mtu yeyote ni vile utaamua kujithamini na kuweka bidii katika kile unachokitalajia kuweka bidii kama utajithamini ni ngumu kukubalika katika maeneo yote ila unaweza kukubalika maeneo Fulani na mengine usikubalike. Hivyo kushindwa kufikia lile ambalo ulikuwa ukitegemea kuwa utafikia.

Ni vizuri utambue kuwa hakuna mtu ambae atakuthamini zaidi wewe unavyo jithamini binafsi.
Ni vizuri utambue utu wa mtu hauwezi badilishwa na chochote hakuna thamani yeyote unaweza kubadilisha na utu wa mtu akipo wala hakuna kitachotokea.

Tambua utu wako ndio thamani yako, utunze ili uweze kuendelea kuthaminiwa.

Ishi maisha ya kupandisha thamani yako siku baada ya siku na sio kupunguza thamani siku baada ya siku, wewe ndio mwenye hatima yako na wala hakuna mwingine ataweza kuchukua thamani yako.



Imeandaliwa na;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



“BARIKIWA……….sana”