MSAMAHA
Hili ni moja ya jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu mahali
ambapo anakosewa anapenda aambiwe samahani na mahali anapokosea anabudi kuomba
msamaha na katika haya yote mawili
kunakukubaliwa na kukataliwa pia kuna hali
ya kukubali au kukataa, japo mtu yeyote anayeomba msamaha kutoka moyoni hasa
pale anapoona kweli amekosa utazamia kusamehewa na hali ya mwanzo kurudi tena.
Na yule anayesamehe anategemea jambo lililotendeka alitajirudia tena na itakuwa
amejifunza kutokana na makosa.
Jambo hili sio swala la kuzoelea kwakua ni jambo
ambalo linatokana na mtikisiko ndani ya mausiano yenu na kuhatarisha mmomonyoko
wa hali ya kuhusiana kwenu japo wakti mwingine inasababisha hali ya kujuana
zaidi na kutambua tofauti zenu na mapungufu yenu na kujua kuwa kuwa huyu yuko
hivi na wala si hivi nilikuwa nikifikiria.
Na mtu ambaye hawezi kuomba msamaha wakati kweli
amefanya makosa basi ni mtu anayetambulika kuwa anakiburi na ajali maumivu ya
wengine na haoni uhitaji wa mwingine katika maisha yake hivyo jamii kwa mapana
yake umchukulia kuwa ni mtu ambaye anayeweza kuanguka wala hata
dawa(ataangamia).
NINI
MAANA YA MSAMAHA,
(a) Msamaha ni
ni hali ya kumbeba kristo ndani ya moyo wako pasipo kuangalia/kuruhusu mwanadamu
au kundi la watu au mtu mmoja anataka/wanataka kubebwa ndani ya moyo wako.
-ukweli jambo lolote ambalo
linakuumiza basi linapeleka kitu kutuama ndani ya moyo wako lakini ni hali ya
kuzuia kwa jambo lolote lisipate nafasi ndani ya moyo wako basi liwe na sehemu
nyingine lakini si katika moyo wako binafsi inaweza kuwa katika akili yako na
ikapata ufafanuzi na ikaishia hapo.
-msamaha ni ishara ya kumpenda
Mungu kuwa kitu ambacho kizunguke ndani ya moyo wako sikuzote, mambo ambayo
Mungu atayafurahia akiyaona yakizunguka ndani yako siku zote kwa ubora na
ustawi wake tu.
-unapoamua kusamehe ukweli ni kwa
faida yako kwakua unaiweka huru nafsi yako mbali na mgandamizo pamoja na msongo
wa mawazo ndani yako na hatimae kutofanikisha au kutikuwa na hali ya utendeaje
ulikatika ufasaha.
Mithali
4:23
-utaweza
kuulinda moyo wako endapo tu utafanikiwa kwa kiwango cha juu cha kristo kukaa
ndani yako na kupata nafasi inayostahili, kwa kua yeye ukimpa moyo wako atautunza
moyo wako kuhakikisha haujeruhiwi kwakua ukijeruhiwa yeye atafurahi kukaa na
wewe katika hali ya moyo kuwa chini au moyo wenye hofu.
Lazima utambue pindi utakapo mbeba
mtu badala ya Mungu ndani yako basi utaongzwa na mtu lakini ujue hakuna hatima
yako iliyo bebwa na mtu mwingine isipokuwa Mungu tu.
(b) Msamaha ni
hali ya kukubali kuonekana sawa mbele za Mungu na huku aliye kukosea au
uliyemkosea akaona hana sababu ya kuomba msahama
Mithali
19:11
Warumi
8:13
-usifanye kitu ambacho kitaleta
faida kwa mtu tu au hasara bali kile kitu kitakusaidia kusonga mbele zaidi
ambacho kitakupa kibali zaidi mbele Mungu.
-hakuna njia nzuri ya maendeleo
ikiwa tu utendaji wako unategemea nitawafurahishaje watu ili nisionekane mbaya,
bali tambua kukuona mbaya au mzuri inategemea mitazo yao kwako na kamwe hauwezi
kuibadilisha kwa namna yeyote bali fanya jambo ambalolitakupa usahihi mbele za
Mungu.
-watu hawawezi kukuelewa kwa kua
hata wao hawajielewi na zaidi ya yote hata wewe bado unajielewa siku
zinavyozidi.
imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
Ni vizuri kusamehe
ili usamehewe……..