MSAMAHA NA MAZINGIRA YAKE;
Kila kitu duniani ilikiende vizuri lazima pawepo na
hali ambayo itasindikiza tendo/jambo hilo kutokea kwa ukamilifu wake, jambo
ambalo alitasindikizwa na hali stahiki jua kitu hicho hakita kuwa na nguvu
katika utendaji wake.
Kila kitu nguvu yake utegemea sana hali gani
inayoisukuma jambo hilo litendeke pasipo hali hiyo jambo hilo linakuwa alina
nguvu.
Tunapozungumzia hali ya kukufanya utende jambo tuna
zungumzia shina ulilonalo katika utendaji wa jambo husika ambalo linakupa nguvu
katika utendaji wake.
Mfano unapokuwa na furaha je, hali gani uliyonayo
inayo sindikiza hicho kicheko kama hali inayokusindikiza katika kicheko sio
sahihi basi hicho kicheko kinaweza kuitwa ni unafiki na hata unapolia je,
haligani inasindikiza katika kilio chako napindi hali uliyo nayo ikatofautiana
na hali uliyokuwa nayo basi uweza kuitwa ni unafiki.
Jambo lolote ili liwe imara utegemea sana shina la
jambo hilo kwa hiyo uimara wa shina upelekea ubora wa jambo husika….kwakua
uimara wa nyumba utegemea msingi wake na ubora wa mti utegemea sana mizizi
yake.
Jambo lolote hili ulifanye katika ubora wake
unahitaji sana ujue kwa ufasaha zaidi kwa nini nafanya jambo hili unapojua basi
pajenga umaana wa wewe kufanya jambo hilo.
MSAMAHA
limekuwa neno la kawaida katika jamii yetu inayotuzunguka, hakuna mtu hajawai
kulitumia hili neno(katika maana ya kuambiwa au kusema) watu imefika wanachoka
kusikia neno hili.
Hili neno limekuwa likitumika sana hatakufika mahali
ambapo kushindwa nani ana maanisha na nani amaanishi imekuwa ikiwa katikati
inaweza kumsamehe huyu kumbe huyu amefanya makusudi na unaweza usi msamehe huyu
kumbe huyu akufanya kwa makusudi ki uhakika hili neno limekuwa liki wachanganya
watu sana kwa watu wako njia ya panda hawajui wafanye nini bali wamekuwa wapweke
kwa kutojua nifanye nini.
Kila mtu anakuwa na maamuzi yake pindi anapotaoa
msamaha wake mwingine atasema nimekusamehe lakini usirudie tena,mwingine usema
nimekusamehe lakini sitaki kukuona ukifanya jambo lilelile tena na kuwa na mtu
Yuleyule tena,mwingine atasema nimekusamehe lakini sitaji tena kukuona katika
maisha yangu tena, mwingine atasema nimekusamehe ila hama mahali hapa au mimi
na wewe tutengane tusiwe pamoja tena na mwingine atasema nimekusamehe ila
tufanye mapenzi mimi nawe ili tuyamalize kabisa au tumalize tofauti zilizopo
kati yetu, au mwingine atasema nimekusamehe ila sasa utakuwa ukifanya hivi au
utakuwa ukinifanyia hivi.
Haya yote ni mazingira mbalmbali ambayo yoyote
anaweza kuwa nayo pindi anapotoa msamaha wake kwa mtu Fulani kulingana na
uhusiano wake.
Kwa muonekano huo neno msamaha limepoteza radha yake
na kwa namna hiyo imekuwa mtu kutoa msamaha wake kwa mwezake ila wa meamua
kuishi maisha ya kisilani na mwezake.
Kuna watu wamekuwa wakisema moyoni mwao siwezi
kumsamehe mtu huyu kwa vile alivyo nitendea ni makubwa na hayaelezeki.
Wengine wamethubutu kusema kuwa hata Mungu anaelewa
kwa hili/lile jambo alilonitendea na hata nikisema ni msamehe mimi mwenyewe
nitajishangaa sana na hata jamii inayo ni zunguka hatanielewa vizuri.
Na wengine husema ni kimsamehe kwa haraka hatasema
mimi najipendekeza kwake au hatasema jambo hili alijaniumiza sana.
imeandaliwa ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
Asante!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni