NAMJUAJE MTU ALIYE
TAYARI KWA AJILI YA MAUSIANO YA KWELI,
Uwa watu hawataki kuhusiana tu bali kuusiana kuliko
na mwelekeo wa manufaa na sio kuhusiana katika muonekano tu wa kuoneka tu
mnausiana. Watu wengi wanapoingia kwenye mausiano katika akili njema( kuwa
wangu katika maisha yangu siku zote ) uwa baada ya kujadiliana na uwezo wa
akili yake katika kupambanua mambo au jambo hilo anapofikia hatma ya kukubali
uwa anajua kwamba bila shaka huyu ni mwanaume au mwanamke wa ndoto yangu hivyo
maisha yetu yatakuwa raha mstarehe lakini wakati mwingi imekuwa sivyo hivyo.
Kila mtu anaamua jambo kutokana na uwezo wa akili
yake katika kupambanua jambo hilo lakini jambo hili uwa aliishii kwenye akili
tu bali linagusa hata hisia za mtu tena katika hali kamilifu sana kuliko
chochote na inawezekana kuwa ni kitu ambacho kinaongoza kukamata maisha ya watu
wengi. Uwa ni matumaini ya watu wengi kuwa na mtu ambaye roho yake itampenda
sana na kumwamini japo sio jambo rahisi kutambua kwani hiyo ni siri iliyo
katika hazina ya moyo wake. Nani kawaida
mwanadamu kubadilika hivyo hatujui kuwa katika hali hii ya kubadilika je!
Atabadilika katika hali njema au mbaya inategemea na muhusika mwenyewe kwakua
dereva wa nafsi ya mtu ni mtu mwenyewe na sio mtu mwingine.
Limekuwa swali la watu wengi hasa walio kwisha tenda
katika mausiano haya ya kimapenzi na hata wale ambao wako mbioni kuingia huko
wamekuwa wakijiuliza maswali na kukosa majibu NI NANI
ALIYETAYARI KATIKA MAUSIANO YA
KWELI NAMI.Kwa hakika hakuna mahali
utaenda nakupata majibu ya maswali haya ndivyo watu wengi wamekuwa wakifikiri.
Na kwakua watu wengi wamekuwa na ndoto za kuwa na maisha ya wawili yaani ndoa
hivyo jambo hili limekuwa ni changamoto kwa walio wengi na pindi wakiangalia
mifano mibaya ya watu walio katika mausiano wapo watu wanauana, wanasalitiana,
wanajeruhiana na wako watu ambao hawana furaha katika ndoa zao na wengi wao
wamekuwa wakikaa kwa shindikizo la wazazi tu na wengine wanangojea watoto wakue
aanze maisha mengine hii ni dalili mbaya na haina mvuto hasa kwa walio wengi
wenye matarajio kuingia huko na wakati mwingine yeye mwenyewe anaweza kuwa
mfano wa yale aliyopitia.
Lakini pamoja na hayo yote bado ningependa kusema
kuwa ndoa ni kitu kizuri sana, ambacho akina mfano wake hapa duniani kwakua
ndani ya ndoa kuna pumziko la kweli linalo kutosheleza lenye kuleta raha
inayodumu, ni mahali ambapo moyo wako unapaweka nafasi ya kwanza hata kuliko
jambo lolote. unaweza kuwa mahali popote ukapewa madini ya gharama kubwa lakini
hapa linganishwi na raha iliyo ndani ya ndoa haielezeki na hata walio katika
ndoa bado wanaona ni ajabu kwa ile amani na furaha ya kweli iliyopo na pia
pamoja na hayo yote bado sio swala la kulikimbilia saaaana kwa wale ambao bado
wanaona wanahitaji muda kwanza na kwa wale ambao hawajaruhusiwa kutokana na
taratibu za jamii zao kwa ujumla wake.
Hapa kuna vitu viwili vya kuangalia kwa umakini
mkubwa:
I.ALIYE TAYARI KUINGIA KWENYE MAUSIANO
II.ALIYE TAYARI KUINGIA
KATIKA MAUSIANO NA
WEWE
Ukiweza kuyajibu maswali haya kwa ufasaha basi ni
wazi utakuwa umeshapata hatua moja ya msingi katika mausiano ya kimapenzi(
ndoa).
I.ALIYETAYARI
KUINGIA KWENYE MAUSIANO
Uwa swala la mapenzi alishurutushwi alipatikani kwa
mabavu au kwa wazifsa wa mtu alionao kwa kuwa na wazifsa huo basi unasifa
kumpata yeyote na kuwa huru kiasi kwamba kile unachotaka ndicho kinafanyika.
Hautakiwi kwakua unakiu na kuwa na mpenzi basi hisia zako zinakuwa na nguvu
katika maamuzi hata pasipo kuyapitisha katika chujio swala moja la kuangalia
hapo ni UMRI si zungumzii tofauti
kati ya wapenzi ambao waliokuwa zaidi ya miaka ishirini mathalani tofauti yao
ikawa miaka mitano(5) au zaidi hapo mimi siingilii na utofauti haujalishi
mwanaume mkubwa au mwanamke mkubwa bali inategemea makubaliano yao wahusika.
Swala umri linakuwa na nguvu kwakua linahusiana uelewa ni kweli kwamba unapo
mdogo uelewa wako unakuwa ni wakitoto tu hata ukipata uelewa mkubwa lakini
hautajua usahihi wa kutendea huo uelewa na kitu kingine UELEWA wa mtu katika mausiano ya kimapenzi tambua naongelea mwenzi
wa maisha na sio swala la kupenda kufanya ngono tu halafu ukahama hama kama
nyumba ya kupanga bali ni maisha ya kujenga familia ya pamoja ila kabla
ujatafakari uelewa wa mwenzako kuhusu mambo haya lazima kwanza wewe uwe na
uelewa sahihi kwakuwa kipimo chako kitategemea na uelewa wako KUPENDA ni kitu
kimoja na UELEWA ni kitu kingine kwakua hichi ndicho unabeba msingi wa mausiano
yenu neno uelewa ni jambo muhimu sana na pindi usipolitilia mkazo wake stahiki ndipo
utakapo tambua umuhimu wake baadae utakapo umekwisha chelewa sana. Katika
kutafuta uelewa hapo hautakiwi umri japo mnaweza kuwa na umri unakubalika yaani
zaidi ya miaka ishirini lakini kama uelewa ulibeba makusudi mema haupo basi ni
vizuri uache kwa ustawi wa maisha yako ya baadae. Na kitu kingine YUKO TAYARI KIMAUSIANO lazima moyo wake
uwe umefunguka kwa ridhaa ya mtu binafsi. Kwakua hili swala linahusisha hisia
utayari wake wa kifikra utaweza kuruhusu hisia zianze kuwa hai, hili ni jambo
la muhimu sana kwani mapenzi ni hiyari mtu katika kukuruhusu uwe mmoja kati ya
wageni wake ndani ya moyo wake na hali hii mwanzo unaweza inaweza kuona ni
dalili nzuri sana ila baadae ukaona tena utayari haipo tena usiyalazimishe na
haya ni matokeo ya uelewa mliokua nao katika mausiano, hakikisha hakuna
kilichomshurutisha mathalani wazazi,ndugu, au kile ulicho nacho. Ni vizuri
akili itambue kuwa kuna kitu kinaitwa mapenzi na sasa nipotayari kuingia katika
bahari hii ya wapendanao na utayari wao binafsi upelekea kila kuthamini na
kujali hisia za mwenzake kwa moyo usio chembe ya uongo bali kweli tupu.
II.ALIYETARI
KUINGIA KATIKA MAUSIANO NA WEWE.
Hapa ndipo tunasema kuwa huyu ndio chaguo langu la
maisha yangu baada mchakato mwendo mzima wa ulimwengu, hapa hautuzungumzii kuwa
mtu kuwa na UELEWA au YUKO TAYARI KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI bali hatua hii
sasa uthibitisho huyu ni wangu na wala si wa wengi. Hatua ndio inapelekea watu
kufa, majeraha na mambo mengine mabaya yanazaliwa hapo kwakua kunamategemeo
waliokuwa nayo na matarajio ya maisha bora ya maisha bora ya hapo baadae.
Nawezaje
kumtambua sasa!!!!!!!!!!!!
(a)anakuzungumziaje?
Kama kweli kitu kimemla moyo wake uwasahau kukuzungumzia
sio mkiwa wote bali hata mkiwa hampo wote bado atakuwa kero kwa wenzake hata
itawafanya marafiki watafute kukujua huyu ndio nani? Mara nyingi inakuwa
uthibitisho katika kupigia simu mara nyingi na meseji zi sizo koma na pasipo
kujua ni wakati wagani usiku mchana au usiku au unafanya kazi gani anachojali
ni kufurahisha hisia zake juu yako na hali hii inawakumba watu wote sio upande
mmoja kila mtu anakuwa anakiu na mwenzake. Japo mnapoanza si vile mtavyokuwa
mkiendelea, utofauti unaweza kuwa na nguvu na kupunguza hile kasi yenu na
kuanza kulaumiana sana kwa huo utufauti hua unausishwa na uelewa usio sahihi
kuhusu hayo mausiano.
(b)lazima ajione yeye ndio wewe
Sio ile kwenye meseji tu ni hali inayoishi kuonekana
pasipo kuko a yenye kudhihirika hata katika kutoa zawadi mmoja na mwenzake.
Lazima iweakiona unafuraha kwakile alichokifanya hicho ndicho kicheko chake na
hata furaha yake.
Lazima aone kuwa thamani yake sio bora kama thamani
yako kwake na hivyo wote mjione hivyo kwakua kila mtu ana muona mwenzake ndio
furaha ya siku yake ila isiwe sinema uwe ni moyo unaongea na huku ukijua kile
unachokiongea kwa akili timamu tena katika hali ya kupenda.
(c)mapenzi yenye kumuhusisha Mungu
Mapenzi ameyanzisha pale edeni alipomtengeneza eva
kwa ajili ya ajili ya adamu, yeye ndio fundi sahihi wa kuboresha mapenzi na
kuleta chachu lakini huu utundu wa sasa katika ulimwengu tulio nao sasa ndio
matokeo kuvunjika saaaana katika mausiano ya kimapenzi tambua kesho yenu
hamuijui basi mapenzi yenu ya mtambue Mungu kwa udhati ili yeye alete Baraka na
furaha katika maisha yenu tangu sasa hadi milele AMINA.
Imeandaliwa na;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“BARIKIWA ………SANA”