Alhamisi, 12 Septemba 2013

MOYO ULIO JERUHIWA



MOYO ULIO JERUHIWA
 
Moyo ni sehemu muhimu sana katika mwili wa binadamu, na jeraha lolote linaweza kuathiri maisha yako kwa kiwango fulani mathalani mtu anapo vunjika mguu au kujeruhiwa hakika ilo jeraha litaweza kumfanya 

kushindwa kufanya jambo fulani kwa muda fulani halafu baadae hali ikarudi kuwa hali ya kawaida vilevile hali hii inaweza kutokea ikaathiri sehemu yoyote katika mwili, lakini sio jeraha la moyo hili ni jeraha ambalo kutibika kwake uwa linahitaji uangalifu wa hali ya juu sana.

Kitu kikubwa kinacho fanya majeraha katika moyo ni MAUSIANO. Tuangalie kwa namna ipi mausiano yanaleta majeraha katika moyo kwa kuangalia aina ya mausiano.


Mausiano kazini!

Hii ni sehemu moja ambayo moyo unaweza kujeruhiwa na kusababisha maumivu katika moyo  kwa kiwango kikubwa inaleta huzuni na hata magonjwa kuzidi kushamili katika miili yetu.

Vipo vikwazo ambavyo vinakuwa vinatokea kazini inaweza kuwa miongoni mwa wafanya kazi wezako au bosi wako.

Na tatizo kubwa linakuwa pale tu kila mtu anapotaka kutimiza maslahi binafsi na pindi anapokosa anaweza fanya jambo ambalo likaleta pigo kwa mwingine.
 
Ni wazi kuwa pindi moyo wako unapo jeruhiwa basi utendaji wako unashuka na ufanisi kupungua.
Sio jambo ambalo mtu analitegemea kuwa litatokea bali pindi litakapo tokea linaleta mvurugiko katika maisha yake kwa ujumla wake.

Pindi unajeruhiwa kazini katika Nyanja ya kimapenzi (hali ya kutaka kushirikiana kimapenzi pasipo ridha ya mtu binafsi) na Nyanja ya kutofurahia mafanikio yako hivyo upelekea kufanya uchochezi wa wewe kufukuzwa kazi au kufanya kazi katika mazingira.
 
Wako watu wanafanya kazi katika moyo ulio jeruhiwa wanavumilia tu, kwa sababu utaishije! Na hili uishi unahitaji hela hivyo unahitaji kazi ambayo itakuwezesha kupata fedha kujikim kimaisha na watu waliokaribu yako wanahitaji msaada wako. Mtu katika hatua hii anawaza mengi kuacha kazi, kubadilisha kazi na mengine mengi.


Mausiano ya kimapenzi!

Hili ni jambo ambalo limesababisha maumivu mengi katika jamii hii ya leo, sio kitu cha kushangaza mtu kubadilisha mausiano ya kimapenzi mara nyingi katika kipindi kifupi sana.
 
Kama pange kuwa na hospitali ya majeraha yanayo sababishwa na mausiano ya kimapenzi hospitali zinge jaa sana na hata kukosa nafasi ya kuwaweka wengine.

Ki ukweli mtu anapoingia katika mausiano haya mazuri matamu zaidi ya asali na chochote kinachofanana na hayo anatumaini kusonga mbele na kuishi ambayo yalikuwa ndoto yake tangu alipo kuwa kijana mdogo.

Majeraha haya yamepelekea watu kusema sihitaji kusikia mwanaume akinitongoza, na kamwe sitatumia muda wangu kufikiri kuhusu mwanaume/wanamke na wengine hata kujiua.


 

Majeraha yanayotokana na mvunjiko wa mausiano haya yamekuwa yakiongezeka siku baada ya siku kadili dunia inavyoenda ndivyo majeha haya yanazidi kuchukua nafasi katika sura mbalimbali, na kupelekea imani ya watu kukosa kuamini kama kuna mapenzi ya kweli zaidi ya pesa na muonekano mzuri wa mtu.

Sababu kubwa na mchafuko wa mausiano ya namna hii ni kutoishi maisha yenu bali ya watu wengine! Ambao hamuwajui, hivi sasa mausiana haya yamekuwa ni maonyesho (fasion), sanaa na mashindano na hata kujilinganisha (wivu pasipo akili).

Haya mausiano yamejenga historia katika maisha yao ambayo hawawezi kusahau bali imebaki jeraha ndani ya maisha yao.

Hali hii iepelekea kupoteza maana ya ndoa, wamefanya kuwa ni jambo ambalo la kuangaliana baadae kila mtu aendelee na mambo yake lakini sio jambo ambalo Mungu amelikusudia.
Napia watu wengi wanaingia katika ndoa sio kwa ridhaa yao wenyewe bali kwa shinikizo la wazazi, ndugu, jamii au rafiki.

Na hata kuchukiana pasipo kuangaliana mpate kuchukua uamuzi wa busara. Na hali hii sio kwa ndoa ambazo zinachipukia bali hata kwa wale waliotayari katika ndoa pamekuwa na shida kubwa sana! Kwa maana nyingine ulimwengu huu wa wapendanao umechafuka sijui utarudi katika hali hile ya awali.

Sasa hivi sio ajabu baba kufanya mapenzi na mwanae, mama kufanya mapenzi na mototo wake na hata watu wenye umri mkubwa kutembea na watoto wenye rika moja na wajukuu zao.

Mapenzi yamekuwa pesa, mfumo wa mapezi tulio nao hauna mfano hatutofautishi uchumba na ndoa kila mtu anafanya kwa namna anavyoona yeye ajali usahihi wa jambo hilo.
 

Kiukweli ndoa imepoteza thamaniyake japo mbwembwe zimeongezeka Sana hasa katika sherehe za harusi. Sasa hivi ndoa ni kukubali mateso, maumivu kutengwa na kufanyiwa jambo ambalo linapoteza utu wako na linaathiri maisha yako kwa ujumla.

Ndoa zimeongeza gharama na sio kuongeza upendo!!!!!!!!!!
Ki ukweli misingi ya mausiano ya kimapenzi haipo hivyo imekuwa rahisi kuvunjika kwakua hakuna nguzo za kushirikilia hazipo.

Watu wameona vyema wajifanyie mapenzi wenyewe kuliko kuolewa au kujiingiza katika mausiano ya kimapenzi.

Ni wazi usipoelewa misingi ya ndoa na kuifuata kamwe hauwezi ukawa na ndoa imara kwani hii iko wazi sana kile unacho kipanda ndicho utakacho vuna, usipande bangi ukategemea kuvuna mchicha!!!



Mausiano ya kijamii!!

Mbali na mausiano hayo yalitangulia pia moyo uweza kuumizwa kutokana na mausiano ya jamii inayokuzunguka.
 
Jirani yako anakuonaje wewe binafsi unawaza nini juu yako na kweli anawaza mazuri juu yako au yuko na kujitanguliza binafsi.

Jamii inahusisha na watu wa karibu pamoja na wazazi wako na wale unaoshirikiana (rafiki) ni kwa namna ipi mitazamo yao na vitendo vyao vinavyo asili maisha yako.

Namna wanavyo tumia mawazo yao kutawala utashi wako ambayo yamejengwa katika misingi yao binafsi yanayo nyima uhuru wako katika kufikia hatma ya maisha yako. Japo sio kila mawazo wanayokupa usiyape nafasi ndani yako.

Majeraha ya moyo ya nakuja pale tu wanapo vunja ndoto yako nzuri na kukupa ndoto yao ambayo ni kinyume cha utashi wako na hata kupelekea maumivu ndani ya maisha yako na kutoona umuhimu wao kwako.
 
Katika jamii inayo kuzunguka namna wanavyo changia katika kuhakikisha kurudisha nyuma maendeleo binafsi maneno ya kukuvunja moyo, kujaribu kurudisha nyuma maendeleo yako kuweka vikwazo vile ambavyo unapigana kutoka pale ulipo.

Ndani ya jamii unaweza kufanyiwa vitendo ambavyo vita athiri maisha yako kisakolojia na kimwili mathalani kubakwa, kuvamiwa na kuathiri mwili wako na kuchukuliwa mali zako na hivyo kurudisha nyuma maendeleo binafsi.

Namna jamii inavyo kutendea jua ndivyo wanavyo jeruhi moyo wako hivyo kuendelea kuvumilia na kuendelea kuangamia.


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

Tufanye nini………wakati ujao!!!!!!!!!!!!!!!!!