MWANZO MPYA
New beginning…………………..!!!!
Pindi unapokosea jambo fulani ni vizuri uanze mwanzo
kuliko kuhisi ulipokosea halafu ukakosea zaidi anza upya utajua wapi umekosea
na nifanyeje.
Mwanzo
mpya au ukurasa mpya wa mtu katika kuanza upya maisha yake
ni jambo lenye sura mbalimbali wapo watu wataona ugumu,wengine wataona kuchekwa
na wengine wataona ni kupoteza muda na hata wengine hawataona thamani ya kuanza
upya.
Mathalani nyumba unapoikalabati ni tofauti na mtu
anaye amua kuanza upya katika ujenzi japo ni kweli kuna gharama kubwa sana mtu
ambaye ataamua kujenga upya tofauti na mtu yule ambaye ameamua kukalabati maana
yule ambaye aliye amuakujenga upya atakuwa amejihakikishia uimara zaidi kuliko yule
aliye amua kukalabati.
Hata katika gari lililo karabatiwa sana na yule
aliye amua kununua gari jipya lipi ni suluhisho la kudumu ambalo litakusaidia
kwa muda mrefu.
Wakati mwingi tumekuwa tukitafauta unafuu katika
mambo yanayo tukabili na sio kuliondoa tatizo kwa ujumla wake,na ni wazi
ukitafuta suluhu ya muda ndiyo utayoipata ambalo baadae jeraha litaibuka tena.
Hii hiko wazi hatuwezi kuwa salama kwa sisi kutafuta unafuu kwa kuwa unafuu ni
akiba ya baadae au ni mlipuko ambao unaweza lipuka wakati popotena kwa mtu
yeyote..
Marko
11:15-16
Hata katika biblia tunamuona yesu akisema;
“nitaliboa hekalu hili na
kulijenga siku tatu…..”
Kwanini yesu akusema nililekebishe hili hekalu kwa
kuwa katika kulekebisha kuna uimara mdogo lakini katika kujenga upya kuna
uimara unaodumu milele.
Moyo uliojeruhiwa dawa
ya pekee ni kuanza upya kabisa!!!!!!
Tatizo kubwa watu wanapo umizwa moyo au kujeruhiwa
mioyo basi wanatumia ujanja na kasi katika kutaka kuziba nafasi zilizo kuwa
wazi!
Uwa hawatumii muda wao katika kutafakari kwanini
haya yametokea na mimi nijipange kwanamna gani ili yale yasifanane na haya, na
hali hii mara nyingi upelekea kuumizwa zaidi na kujeruhiwa na kusababisha
hatimae kujenga majenzi ambayo ni vigumu kuyaondoa kwani hayaondolewi kila
hisi.
Mtu alijeruhiwa moyo kwa kukosa kujua nini cha
kufanya upelekea kufanya lolote ambalo litakuja kichwani mwake utegemea na
uelewa wake kuhusu hayo mausiano haya wapo watu wanathubutu kusema sitamwamini
mwanadamu tena,hata wengine upelekea kujiua…..!
Kama mtoto anzapo hatua ya kutembea kuna kuanguka
lakini mwishoe usimama lakini katika mausiano yanapo vunjika ili uendelee
vizuri ni vizuri uanze upya katika ubora ulio mzuri zaidi na sio kukulupuka.
Namna
ya kuanza upya kwa mtu aliye na moyo uliojeruhiwa!
I.ikubali hali iliyotokea
na wewe ndio muathirika wa jambo hilo.
Tunapozungumzia kukubaliana na hali iliyopo hatuna
maana kuwa ni jambo mbalo umelisababisha wewe la! Asha bali ni jambo ambalo limegusa moyo
wako limeleta matokeo ambayo yameathiri maisha kwa namna moja au nyingine.
Hali hiyo uone sasa tatizo limesha kupata ona Mungu
anatambua majeraha ndani yako na anategemea jambo ambalo jipya lenye utukufu
wake kuzaliwa ndani yako.
Usitumie wakati wako kumlahumu mtu kwani hata
ukimlahumu mtu haita saidia kitu tambua wewe ndio muhusika na maisha yako
kupitia wewe unaweza kutengeneza kesho iliyo bora kama ulivyoitengeneza ikawa
leo kwa vile ulivyo kuwa jana.
Lazima utambue wote wanaweza kufarahia watakapo
kuona uko vizuri na wala si wakuone vibaya lakini ni Mungu tu anayeweza
kukutengeneza vile tu utakiwavyo kuwa.
Watu wanaweza jua uko kwenye tatizo lakini namna ya
kutoka hapo kunaweza kuwa shida wakati mwingine baada ya kutoka wanaweza
kuongeza jambo likawa ni tatizo kubwa.
II.kubali kuwa huo ndio
muonekano wa maisha yako ya nyuma.
Tambua kuwa hakuna mtu asiye historia yake na kuna
uwezekano wa kuwa tofauti hivyo kubali kuwa hiyo basi ni historian a wala sio
jambo jingine.
Hakikisha nyuma isikusumbue bali mawazo yako ya
mbele ya chukue nafasi na kupanga mikakati ya namna ya kuboresha kesho.(kitu
ambacho kikusumbue katika kichwa chako namna nawezaje ni kufanya kesho yangu
ikawa tofauti na leo na huku ukiona uwezo wa kufanya jambo upo pasipo na shaka
yoyote kwakua una mwamini Mungu yeye asishindwa).
Hakikisha usiishi maisha ya unyonge kwa kuwa huruma
ya kibinadam haina hatma njema katika maisha yako binafsi.( binadam wote
wanahitaji faraja maisha yao yote hakuna siku hatatosheka)
Ni wewe unaweza fanya jambo likapita au jambo
likadumu ndani ya maisha yako kwa kulipa nafasi.
Jua kwamba hiyo ni histori ya maisha ambayo ni tofauti
na mwingine hivyo jua inahitaji ibaki kama kumbukumbu lakini isiwe dira ya
maisha yako au ikazalisha maisha ya uwoga katika kuchukua maamuzi mazuri katika
maisha yako.
Ni lazima mtu ili awe wa maana sio lazima alikuwa wa
maana toka awali bali wapo walikuwa hawana historia ya kuvutia na mwisho wake
ulikuwa ni ushuhuda mzuri.
III.utambue mtazamo wa
Mungu juu yako.
Unapo muona Mungu ni zaidi ya baba,mpenzi,rafiki hivyo
ndivyo alivyo hama kwa hakika hakuna mfano wako na wala hatatokea.
Biblia inasema;
-sikuja kwa ajili ya
wenye haki bali wenye dhambi ili wapate kutubu.
Na vilevile inasema tulipokuwa wenye dhambi Mungu
alitupenda zaidi, huna haja ya kuona wanadam wanavyo kuona basi ndivyo Mungu
anavyo kuona.
Na Mungu sifa kubwa anaangalia mwisho wenye ushuhuda
huwa angalii ulianzaje bali anangalia umemalizaje na sio jambo jingine,
mathalani katika riadha mshindi anatambuliwa mwanzo wa mbio au mwisho wa mbio.
Huna haja ya kukata tama bali zidi jua hata kama
mwili wangu najiona sifai kuwa mme/mke
jua bado unafaa sana kwa Mungu nae anaweza kukutengeneza ukawa bora hata kuliko
mwanzo.
Kama ni msomaji wa biblia mzuri basi utamtambua
AYUBU jinsi kesho yake ilivyokuwa ya kutamanika kuliko jana yake.
Yakobo 5:11
Ni vizuri kutambua kuwa anaweza kubadilisha kesho
ikawa nzuri kuliko ni wewe na Mungu na
wala si mtu mwingine.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042
or james.adili19@gmail.com
“TUNAKUTAKIA
MWANZO MZURI”
We
wish you good beginning………….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni