Ijumaa, 14 Machi 2014

FAHAMU NGUVU ILIYO NDANI YA AGANO



NGUVU YA AGANO

Ni neno la kawaida ambalo limekuwa likitumika katika jamii yetu kama neno ambalo linaashiria mtu kumaanisha kwa kile alichokusudia kukisema kuwa ndio kweli na ndicho anacho maanisha na kamwe hawezi kukiuka yale makubaliana ambayo wamekubaliana.

Ninapozungumzia neno hili AGANO lina maana zaidi watu wanavyofikiri au watu wanavyolitumia lakini ukweli ni kwamba neno hili ni zaidi ya kukubaliana maana hili neno lina beba kifungo kisicho onekana lakini kina athari kubwa sana endapo tu usipozingatia hilo agano ambalo watu wanaanzisha halafu hawalizingatii.

Ukweli katika duniani asilimia kubwa watu wanapitia katika hali ngumu ya maisha na magonjwa tofauti ambayo majina ya hayo magonjwa hayajagundulika bado lakini inawathiri lakini sababu kubwa ni kutoheshima agano.

Agano linauwezo kukutengeneza kuwa katika hali njema au mbaya kutokana vile utavyolienda hilo agano na uwezi kumlaumu mtu bali itabidi ulilaumu hilo agano.

Tunapozungumzia huwa atuzungumzii swala ambalo lina nafasi ndogo katika maisha ya mwanadamu bali ni jambo lenye nguvu ambalo laweza fanya jambo ambalo uwezi kuamini kama yale yaliyo kupata ni matokeo ya agano.

Katika jamii kuna nadharia mbalimbali zinazohusu Agano:

i.Agano la ndugu

hili agano ambalo likowazi haupangiwi bali inakuwa kitu kilichofanyika ambacho akiitaji usaidizi wowote bali  hali hiyo imewekwa na Mungu mwenyewe kuwa wewe na ndugu namna mnavyotakiwa  kuenenda.

Watu ambao hawalipa nafasi na kuliheshima hili agano lazima matokeo yake ya taambana katika maisha yake, mathalani mtu anauwezo wa kuwasaidia ndugu zake ataki kuwasaidia au hawatambui tena kutokana na hali aliyokuanayo sasa. Wengine wanawakataa wazazi wao,ndugu zao hali hii itapelekea maumivu makali katika mioyo ya ndugu zake na hivyo malipo hayo lazima ayavume kwa mtu ambaye amekiuka agano ambalo lililokuwepo tangu kuzaliwa kwako katika jamii hiyonayo.

Hili agano lipokwenye damu moja kwa moja halina mjadala umeshaunganishwa ni wewe kulitendea kazi ipasavyo lasivyo litakuweka katika mazingira usiyoyapenda.

ii.Agano la urafiki

haya ni maagano ambayo ni rahisi kuingia na pia ni vigumu kuyasimamia,haya maagano yanakuwa nalengo la kufanya uimara wa mausiano ya weze kudumu sikiu zote.

Na hiki tokea mwingine haonyeshi ushirikiano wa uhakika katika uthabiti wa kutoa hayo maneno ya kuingia agano mwingine anajisikia vibaya.

Ukweli maagano sio kitu kibaya kuingia lakini ni jambo ambalo linawafunga katika mausiano yenu hata kama nyinyi binafsi mnaona ni jambo kupita tu.

Japo katika jamii yetu hali hii kumaanisha katika kuingia agano imepungua sana kiasi kwamba watu hawaoni umuhimu wa swala hili lakini ukweli kwamba ndilo swala ambalo linawatesa wengi hata pasipo kujua kwanini nateseka.

Maagano mnapoingia kuna vitu vinashirikilia huo muungamaniko wenu mathalani vitu vinavyoonekana na visivyoonekana kama vile miungu na hata hali mbalimbali ambazo zinashuhudia katika makubaliano yenu.

Watu wengi wanapovunja maagano yao kasha maisha yao yakaendelea kuwa mazuri basi ufikiria hakuna athari yoyote lakini kumbuka athari ziko nyingi ikiwemo hali ngumu ya uchumi,kufungwa kizazi,kutotulia na mtu moja(mke/mme),magonjwa katika mwili wako yasio koma na hata kuibiwa kuharibikiwa na mimba ya mara kwa mara. Wengine wanasema mikosi hivyo utaka kwenda kwa waganga ili kuondoa hiyo mikosi na njia nyingine nyingi lakini katika yote bado yanabakia palepale.

iii.Agano katika uchumba(ndoa)

hili agano la tofauti sana kutokana na radha yake hili ni agano ambalo haushurutishwi ila unakwenda na kufanya mwenyewe tena bila kuona ugumu wowote.

Katika madhara makubwa yanapotokea pindi maagano yanapovunjika aina hii ya maagano yanakuwa na matokeo mabaya sana ambalo linawezafanyika jambo ambalo alijawaitokea alijawaifikiriwa.

Katika hali hii mtu wa namna yoyote anaweza akafanya jambo ambalo jamii ikabaki kushangaa na watu wengine wasione maana ya kuingia mausiano katika aina hii ya maagano.

Katika hali ya kiuchumba mtu uingia katika maagano ambayo hayasemeki kwenye aina nyingine kwakua kuna muungamaniko wa maisha ilikutokeza pamoja na kuna namna ya kushirikiana ambavyo ni ngumu kushiriki na mtu yeyote kwakua uchumba ni mahali ambapo uumbaji wa Mungu unafanyika.

Hatua hii maagano yanapovunjika ni aina hii pekee ya mausiano ambayo mtu uweza kuona bora afe kuliko kutokua tena maagano na mtu husika.


AGANO  LA  MUNGU  JUU  YA  MWANADAMU…

Mwanzo 9:8-17,15:18

Hili ni agano amblo limekuleta duniani ambalo lina nguvu kubwa katika kuyafanikisha maagano yote.
Kama ilivyo kumweshimu Mungu ni kuheshimu maagano yake juu yako na hakuna namna ya kumuheshimu Mungu nyingine mbali na kuheshimu maagano yake, hauwezi kusema na muheshimu mtu wakati ambao uyazingatii maagano ambayo mmekubaliana.

Japo imekuwa ni jambo ambalo mtu analiona kuwa kawaida kulifanya pasipo kujali nini hasa ya kumweshimu na kumthamini mtu.

Wengi wanavunja maagano sio kwasababu hawataki kuendelea na mtu au na jambo Fulani bali ni ahali yakushindwa kuyazingatia yale makubaliano. Mathalani unapokuwa kazini pale ubora wako na uimara wako unatakiwa uonekane pale katika kuzingatia maagano mliyokubaliana na pindi kama ujakubali kuyatekeleza hayo makubaliano basi unafukuzwa kazi.

Hatuwezi kuishi na Mungu vizuri kama hatutekelezi yale maagano yetu tuliyonayo na yeye kwakua yeye anayaheshimu sana maagano yake kwa kiwango cha juu sana,

Namna Mungu anvyoheshimu maagano aliyoyaweka;

Mwanzo 8:20-22, ..Mungu akasema moyoni mwake,sitailaani nchi tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya……muda nchi idumupo,majira ya kupanda na mavuno,wakati wa hari,wakati wa kaskazini na wakati wa kusi,mchana na usiku, havitakoma.

Haya ni maneno ambayo Mungu mwenyewe ameyayasema na anayasimamia mpaka leo kama alivyosema lile ambalo alilifanya kipindi cha nuhu baada kuachilia gharika kubwa duniani hivyo Mungu ameto nadhiri yake kuwa hatafanya tena jambo hilo hata kama wanadamu wamemkosa kwa namna yoyote.

Dunia ilipoangamizwa makosa yaliyofanywa na wanadamu yalikuwa si makubwa kuliko yanayofanywa na wanadamu wa sasa kwakua dunia tuliyonayo sasa mambo yanatisha yanapoteza thamani ya utu wao,Mungu ananafasi ndani ya mwanadamu imekuwa chafu haivutii lakini bado Mungu anaiheshimu agano lake aliloliweka na nuhu.

Mwanzo 9:13

Kwa hakika yeye ni mwaminifu kwa lile agano na analisimamia kwa hali yote aijalishi uchafu umezidi au la! Lakini bado ameishikilia agano aliloliweka.

Na Mungu ameweka upinde mawinguni ili izidi kumkumbusha yeye kwa hile agano lake, japo tunajua Mungu anatabia ya kusahau kama wanadamu wengine lakini ameweka upinde mawinguni ili asije akaghairisha akaiangamiza tena dunia katika maangamizi makubwa yasio elezeka.

Namna Mungu anavyolisimamia lile agano lake kwa kila namna kuhakikisha inakuwa vile alivyokusudia ni muhimu binadamu yeyote anaweka agano na Mungu lazima ajue kuwa huyu ni Mungu ambae anasimamia agano lake kwa ukamilifu sana hivyo lazima roho hiyo iwe ndani yake ili kwenda pamoja kwa moyo uliotayari kwa gharama yeyote.

Mungu ili akutendee anangalia namna unavyoweza kulizingatia agano lake kwako hivyo usipo li heshimu agano hilo Mungu basi usitegemee kabisa Mungu akakuangalia wewe binafsi kama uzingatii agano lake nawe.

Na kila agano linaenda na Baraka zake hivyo usipolitimiza agano basi sahau juu ya Baraka hizo kukuandama.

Katika dunia ya sasa watu wengi wanasema wanamuogopa Mungu lakini hawana haja na agano lake Mungu juu ya maisha yao hii haiwezekani kwakua hali hii ni sawa na kusema na muheshimu sana na kumpenda mtu lakini yale mliyoweka agano nae halitilii maanani.

Na pindi agano lisipozingatiwa basi uhusiano unavunjika pasipo shaka ni kama vile katika ndoa ikiwa wanandoa wasipozingatia agano lao basi ndoa hiyo kinachofuata ni kuvunjika kama tu wasipokubali kubadilika.

Ni bora umsahau mtu kuliko kusahau agano mliloweka itakuwa mbaya na hutaamini yale ambayo yanayoweza kutokea katika maisha yako. Ukweli mtu anaweza usione kuwa ni jambo la kawaida jua kitakachokusumbua sio mtu bali ni hile agano(NGUVU YA AGANO).

Kuna agano la Mungu juu ya isaka kwa ibrahimu

Mwanzo 17:15-17(1-23)

Hali hii ibrahimu na kwa sara lilikuwa ni jambo gumu sana kukubalika kwa namna ya akili ya kibinadamu wakati mwingine unaweza ukahisi hili jambo kufanyika litakuwa ni ngumu sana na kuona kweli Mungu anaweza kutimiza ahadi hii.

Bado Mungu alionesha kuwa uwaminifu katika kutekeleza lile lililokuwa gumu kwa namna ya mwili lakini yeye alifanya mwenyewe kwa ukamilifu sana pasipo na kitu kinachoweza kumzuia.

Mwanzo 22:1-15

Mungu anapenda mtu ambae anamsikiliza kwa umakini sana na kulifanya kwa ukamilifu sana pasipo hofu bali kwa kutii na kupenda pamoja na moyo wa kuamini uwezo wake.


Natunzaje Agano la Mungu; 

Hapa ndipo pahali ambapo natamani sana kusema ndio msingi wa somo hili na ukielewa hapa unakuwa katika nafasi nzuri sana.

Mwanzo 39:1-12(6,9)

Hapa tutamwangalia kijana mmoja anaitwa YUSUFU kama kijana ambaye alifanikiwa kulitunza agano lake na Mungu kwa ukamilifu wake na ustawi usio wakawaida.

i.Kubali kupata aibu ili Mungu apate heshima

mambo yaliyo katika dunia hii yanataka wewe upate heshima na Mungu aibike inategemea wewe uko upande upi kuchukua heshima kwanza ili upate aibu au kuchukua aibu ili upate heshima.

Unahitaji kujua kwamba yusufu angeweza kufanya jambo lolote katika kupata nafasi nzuri ambayo dunia ingempa lakini alitambua jambo moja……..Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkose Mungu!!!!!!!

Japo alikuwa njia ya panda Yule mwanamke kutokana na wadhifa alikuwa nao angeweza kufanya jambo lolote hata kumuua, ili yeye asihabike. Pamoja na hayo yusufu alikubali yote yampate ila asimkose Mungu kwakua alitambua hatma ilipo.

Kwa hiyo alikubali hata kufa ila atunze agano mbaele za Mungu.

Ufunuo 2:10b

………..uwe mwaminifu hata kufa,name nitakupa taji ya uzima.


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com


                                        TUNZA  AGANO  ILI  AGANO  LIKUTUNZE.

Maoni 1 :