Jumatatu, 12 Agosti 2013

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA



                                                          NDOA:

Ni vizuri kutangulia kutambua nini maana ya ndoa kabla hujaingiza katika jambo lenyewe kwakua  pindi utakapo tambua inakupa kujipanga vizuri.zipo maana mbalimbali zinazotolewa na mashirika,mila na desturi,kisheria kuhusu ndoa.kiukweli ndoa ndio chanzo cha familia,jamii na hatimae taifa kwa ujumla.hivyo ni muhimu sana kujifunza na kutoa kipaumbele kujua misingi mizuri ya ndoa ili kupata taifa bora, japo jamii ya sasa kunatatizo kubwa la ndoa nyingi kuvunjika na matatizo yake ni mengi mathalani watoto wa mitaani.
                           1st position JESUS

Mambo ya kuzingaatia;
I. sio kila mtu anayekuvutia anafaa kuwa mwenzi wako.
-sio kila kizuri kinachopita mbele yako kinafaa kuwa chako.

II .sio kila mtu aliyekidhi vigezo vyako anafaa kuwa mwenzi wako.                                              -tambua swala la ndoa alihitaji kubahatisha ni swala makini sana lililobeba ukamilisho na mwendelezo bora wa hatima yako.
-ukikosa hatua ya kwanza inaweza kukupelekea kukosea hatua nyingine.

III .sio kila mtu ili mradi ameokoka anafaa kuwa mwenzi wako.
-tambua wokovu ni swala la mtu na Mungu na wala sio la kutazama kwa macho ukatoa maamuzi.
-wako waliovaa sura ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu wa kali sana.
-sio wote wanaoingia kanisani na kutoka basi ameniokoka na anafaha kuwa mke/mme wako.
Ni kweli mtu asiyeokoka anaweza kuwa mwenzi wako lakini kwa special case ambayo anaijua Mungu isiyousishwa na mataminio ya kimwili(fedha,kiwango cha elimu au jinsi alivyo)

IV.sio kila mtu mwenye uwezo (akili,fedha,busara,hekima) anafaa kuwa mwenzi wako.
-Tambua unakwenda kuishi na mtu mwenyewe na tabia zake na wala sio fedha zake na mambo mengine aliyonayo.
Sio wakati wote mtu atakuwa na hekima na busara wakati wote tambua huyo ni binadamu aliye na tabia kamili za kibinadamu.

V.sio kila mwenye uwezo wa chini(kifedha,akili,hekima) anafaa kuwa mwenzi wako.
Tambua mtu sahihi uja kwa mtu sahihi katika Mungu maana yeye ndio anayejua.

VI.sio kila mtu anayejua mambo mengi anafaa kuwa mwenzi wako.
Tambua mtu na mambo yake ni vitu viwili tofauti, unaishi na mtu na wala sio mambo anayo yajua yale yote ni ubinafsi wake.
Kuoa/kuolewa sio sifa bali ni mpango kamili wa Mungu kwako.
Hauhitaji usianishwe sana na  matamanio ya kimwili kwani roho na mwili haviwezi kupatana milele.

VII.sio kila mtu aliyekusudia anafaa kuwa mwenzi wako.
Usitake kulipa jema kwa jema,kwani yeye aliye kusaidia ujui ana malengo gani? Yanalingana na wewe.
Ni vizuri kuonyesha shukrani kwa jambo alilo kutenda lakini zipo namna nyingi sio lazima uonyeshe  shukrani kwa kutaka kuwa mwenzi wako.
Tambua mambo haya hayahitaji haraka kwani yapo na hautapitwa na hatua hii maadam unaye Mungu anaye kukuwezesha.

VIII.sio kila mtu mwenye mvuto/kivutio cha watu wengi anafaa  kuwa mwenzi wako.
Watu wengi wanavyo muona anafaha sio Mungu anavyoweza kumuona anafaha kwako.

IX.sio kila mtu aliyesoma au hakusoma anafaa kuwa mwenzi wako.
Mtu apangiwi bali Mungu anaona kesho yako ndio anakuandalia kwa kupatia mtu sahihi akufahae sasa na hata baadae.

NDOA ni mchanganuo wa mambo mengi yaliyopitiliza na sio jambo moja au mawili ambayo watu uwaza (kustarehe,kucheka na kuburudika)
Ndoa haina ufundi au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine ikiwa inafasi ndani ya ndoa yenu.
Ni vizuri utambue nini hasa maana ya ndoa katika hali ya kiMungu.(kusudi la Mungu katika ndoa)
Hiko tafsiri ya ndoa kwa maana ya kidunia ukiichukua na ukaingiza katika utendaji ni vita viwili tofauti hakika vitapasuka maana havichangamani.
Ndoa si kwakua umetamani tu unaoa au kuolewaau namna ulivyo upanga kwa muda mrefu ndio maana unaoa/kuolewa lakini ndoa ina maana zaidi ya hapo.
Napenda utambue kuwa ndoa sio sifa /ufahari katika jamii ili watambue kuwa sasa wewe ni mtu uliyeoa au kuolewa.
                          Torati 10:20-21
Ni maisha ya wawili yanahitaji mshikamano wa hali ya juu kwani maisha haya yanagharama.
Pamoja na hayo iwe ni kweli Mungu anaweza kuwatengeneza sio mengine.
Hasi kudanganye mtu ndoa si kama wale wanavyoishi bali ni vile na mwenzio mtakavyoishi au mnavyoishi.
Kwani ndoa  nyingi ni tofauti katika ulka,mtazamo na hata matamanio tofauti.

Nini maana ya ndoa hasa?
Ndoa ni muungamaniko wa watu wawili wenye jinsia tofauti(mke na mme) usio na kipaumbele sana matamanio ya kimwili bali katika maisha yaliyo jaa furaha kwa jinsi mlivyo na yenye kibali kwa  Mungu.
    Mwanzo 2:5-25
Kwa maana hii ndoa ni furaha,faraja,kicheko,burudani,matumaini maana Mungu yupo pamoja na ninyi
Kwa hakika haya ni maisha ambayo hutamani yesu harudi mapema.
Kwani mateso mengine shetani uwatesa kwakua hawajui maana ya ndoa.
    Mithali 2:11
Ni kweli ndoa ni muhimu japo si lazima lakini usalama wa maisha yako yaliyo jaa furaha na amani na maono ya maisha ya baadae katika Mungu ni muhimu sana. 
                              I wakorintho 7:1-9(8-9)
Tambua ndoa imara ina tegemea misingi imara sana usitegemee ukaendelea vizuri wakati misingi sio imara.
Ushauri!!!!!!!!!!
Sio swala la kukulupikia japo ni jema
Kwakua,
Jambo sahihi uja kwa wakati sahihi na mtu sahihi.
Ni bora wakuone unachelewa lakini huko katika mpango sahihi wa Mungu kuliko wakuone unaendelea vizuri /unaenda na wakati huku Mungu yuko mbali nawe.
Ni vizuri utambue kuwa Mungu anakupenda na anakuwazia yaliyo mema na mpango mzuri na anatambua na anathamini hisia zako.
                       Yeremia 29:11



Prepared by:
                   Cothey Nelson          – 0764018535 or cotheyn@yahoo.com
                
                  James Adili Katiti       - 0713398042 or James.adili19@gmail.com



 “tunaWAtakia maisha mema katika mungu”




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni