RAFIKI NI NANI?
Rafiki ni mtu wa muhimu
sana,kwakua katika kuwa nae unapata kujua upande mwingine wa maisha yaani nini huyu rafiki yako amepitia katika mwenendo
mzima wa maisha yake na nini anajua kuhusu maisha kwa ujumla wake(mtazamo wake
kuhusu maisha) kwakua pasipo yeye kukutana na wewe usinge ya jua, vilevile
katika kukutana/kuwa na rafiki unaweza kubadili kutoka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine(mchango wake katika kuyainua maisha yako kimawazo au uchumi)
Ni kawaida rafiki mzuri
watu hudumu nae nautamani kuishi nae wakati wote na rafiki asiye mzuri watu
uvunja husiano wao,kwakua hukosa kuona umaana wa kuwa na rafiki pasipo kuona
mchango mzuri katika maisha yake.
Hivi ni rahisi kutambua huyu ni rafiki mzuri au rafiki mbaya
kwakusikia habari zake au kwa kumuona kwa kipindi kifupi?
Rafiki ni mtu muhimu
sana kwakua wako watu waliotoka kimaisha
kutokana na msaada wa rafiki na wako watu ambao hawajatoka kimaisha kutokana
kutokana kukosa rafiki au kukosa rafiki ambaye anayeweza kumtoa mahali alipo na
kwenda sehemu nzuri.
Sikuzote matarajio ya
rafiki ni kuwa nae wakati wote akusitiri katika aibu yako na akukosoe katika
pale unapoenda vibaya na rafiki wa namna hii ndipo utaona umaana wa kujivunia
urafiki wenu,
Ninapozungumzia rafiki
inawezekana kuwa wa jinsia yoyote wa kike au wakiume ili mradi anatimiza wajibu
wake kama rafiki.(rafiki ni rafiki jinsia sio jambo la kulipa kipaumbele kwa
kuwa alina maana unachohitaji ni kupata mtu ambaye anatambua nafasi yake kwako.
Katika dunia tuliyonayo
wako watu ambao wameinuka kutoka na usaidizi rafiki walio karibu sio nyanja
moja bali sehemu yote ya maisha binafsi.
Rafiki wa karibu!
Mtu naweza kuwa na
rafiki aliye mbali na aliye karibu (mtu ambaye mnaonana mara kwa mara) na
kushirikiana katika mambo mnayo yakabili pamoja.
Mtu ambaye athri yake
inawezekana kuonekana kwa haraka ni Yule aliye karibu yako kwakua jambo
atakalofanya litakuwa udhihirisho mkubwa.
Lakini kumbuka kuwa sio
wote unao wapenda wanafaa kuwa marafiki zako, kwakua kunatofauti kubwa kati ya
watu unao wafahamu na watu ambao ni marafiki zako. Japo wote unaweza
kuwashirikisha lakini yako kuna kitu unategemea akifanye ili arudishe matumaini
ndani ya moyo wako.
Vile rafiki yako alivyo
ndivyo atakavyo weka namna yako utakavyo onekana endapo tu kama utamkubali
ndani ya maisha yako, kwakua unaweza kuwa na mtu aliye karibu sana na wewe na
hata mkashirikiana mambo mbalimbali hata ya mwilini lakini usimpe nafasi ndani
yako na wala asi athiri maisha yako.
Iwakorintho 15:33
Ni hatari sana kuwa
narafiki ambaye hakusaidii kukupeleka katika njia ambayo Mungu anataka uende.(udhihirisho
wa urafiki wa kweli haupo katika kusema tu bali ni mchango unao onekana ndani
ya maisha yako)
II nyakati 22:4-5
Mathayo 16:26
Rafiki asiye jua
apasalo kufanya kwako huyo ni sumu sana kwakua kwakua anaweza kukupeleka kusiko
kusaidia lakini kwa rafiki anayetambua wajibu wake kwako yeye anaye weza
kurudisha furaha mahali pasipo na furaha na matumaini pasipo matumaini, kicheko
pasipo kicheko na hata kuondoa upweke na simanzi ndani yako.
Ni wazi rafiki mzuri
ili afanye mazuri juu yako kwanza hauna budi kumtambua halafu ukampa nafasi,
pindi unapokosa kumtambua halafu ukampa nafasi ndani yako anaweza fanya jambo
ambalo litaweka historia katika maisha yako.
Ili mwende pamoja
lazima muwe zaidi ya kuwa pamoja yaani muwe na nia moja katika kukubaliana yale
mtakayofanya katika moyo ulio safi.
Kamwe rafiki yeyote
ambaye amjaambatana katika kunia mamoja ni vizuri kuachana nae kwakua uwezi
kumsaidia kwa kumvumilia/kwa kuvuta subira atakuharibia au kukuchelewesha.
Lazima upate rafiki
ambaye mtazungumza mambo ambayo yatapata kibali kwa Mungu katika maendeleo yenu
binafsi na hatma njema iliyojaa Mungu mbali na hapo utapotea hakuna mapumziko.
Mithali 14:12
Sifa za rafiki aliye bora:
Kumbuka kila rafiki
ambaye unae anao mchango katika kukutengeneza au kukuharibu jambo hili lazima
ulichukulie katika uzito wake.
Maandiko ya mungu yanasema,
“ndege wanaofanana ndio
wanao ruka pamoja….”
Asikudanye mtu siku
zote kile unacho kisikia, kukiona na kikipata nafasi ndani yako kinafanyika
sehemu ndani ya maisha yako.
Kama unataka kuwa mtu
wa maana lazima uwe na rafiki ambae ni wa maana vile rafiki yako alivyo ndivyo
atakavyotoa mchango wake.
I .awe
anamjua Mungu.
Tambua kile alichonacho
rafiki yako ndicho atachokupa sio kitu kingine ambacho hana, ni vizuri maisha
yaonyeshe kweli anamuhofu Mungu,
Sio rafiki kila jambo
yeye ni shabiki tu ajali jambo hili lina mpendeza Mungu au la! yeye ukulupikia
maadam lina manufaa kwake.
Tambua sisi sote
tumetoka kwa Mungu na kwa Mungu tutarudi, mambo ya dunia yanapita japo yanavutia
ila angalia yasikutenge na Mungu kwakua Mungu yupo mahali pote na hata dumu milele.
Hivyo rafiki mzuri
pamoja na mambo mengi ni mtu anayekukumbusha kuwa umetoka wapi?
“Watu wawili hawawezi
kwenda pamoja isipokuwa wamepatana”
Hakikisha mwenendo
mnatembea ni mwendo ulio na nuru ya Mungu ili mambo yenu Mungu hayafanikishe.
II.anayejiheshim
Ni vizuri huyo rafiki
lazima ajue maana ya heshima na anayejiheshim na anawaheshim watu wengine.
Tunapozungumzia
hatuzungumzii ustahara wa kusalim (kupiga goti, sauti ya upole) ni zaidi hapo
heshima ni namna unavyowaelewa watu na utu wao.
Anachokifanya ndicho
hicho anachokimaanisha hana utofauti wa kauli ya mdomo na moyo wake.
Thamani ya watu kwake
huwa haijengwi na kipato cha fedha, muonekano au maneno mazuri ambayo
yanazungumzwa na mtu husika.
Ni mtu ambaye anawajali
watu Kama anavyo mjali Mungu kwa kuwa watu tumetoka kwa Mungu kumpenda Mungu
pasipo kuwapenda watu ni bure.
Luka 2:52
Japo wanadamu wote sio
wema bali wewe fanya wema kasha uende usingoje matokeo.
Maandiko yanasema:
“Utampendaje Mungu
usiye muona wakati unamchukua jirani yako……”
Katika dunia ni jambo
la kawaida kumchukua binadamu wenzako halafu ukasema nampenda Mungu.(huwezi
kuwapenda wazazi halafu ukawachukia watoto kwakua watoto ni sehemu ya wazazi)
Mathayo 5:43-48
III.kielelezo safi
Rafiki mzuri lazima
mwenendo wake unakuwa mwelekeo mzuri na sio lazima awe kiongozi wa jamii,japo
anaweza kuwa kiongozi wake binafsi.
Ni mtu ambaye anajua
iko jamii wanahitaji kujifunza kupitia yeye inategemea na rika alilonalo
Kielelezo safi ni kitu
muhimu sana kwakua atakuachia mambo ya mazuri ambayo utayatumia kaika maisha
yako.
Ni kweli unaweza kuwa
na watu wengi wasiwe kielelezo kwako lakini asiwe rafiki kwakua ana nguvu ya
kukushusha au kukuimarisha.
Lazima kielezo safi
ziwe sifa ambazo binafsi anazizingatia kwa mwenendo mzima wa maisha yake
binafsi.
Mathayo 5:16
Japo kuna watu wenye
maadili mema lakini pamoja na hayo unahitaji kuwa na Mungu ili akuwezeshe
kudumu katika kielelezo safi kwani katika dunia ya sasa unaweza kukutana jamii
wakabadilisha ule mfumo wako wa maisha kwa ujumla wake.
Hakikisha awe anaongea
mambo ambayo yanajenga yaliyo na mufaa kwa jamii inayo mzunguka, sio mtu aliye
jaa majungu na visasi ndani yake,
IV.mwazi,mkweli
Lazima anapokuwa na
wewe ni mahali ambapo moyo wake unakuwa na nguvu na kusonga mbele kwa hali hiyo
ni lazima awe mwazi kwako( hali ya kweli itoke ndani yake aseme kanakwamba
anajiambia mwenyewe)
Hii ni moja ya nguzo ya
kweli katika maisha yenu kama hamna hali
hii jua kwamba urafiki wenu unauhalakini au dosari au kutoaminiana.
Lazima muonane ninyi ni
zaidi ya kila kitu pindi mnapo kutana mnajenga vitu ambavyo vinakuwa na faida
katika maisha yenu binafsi.
Kama rafiki ambaye sio
muanzi jua huo urafiki wenu unadosari kuwa makini au jipange kwa lolote kutokea
wakati wowote.
Uwazi ni ishara kubwa
sasa mmeanza kuingiliana katika urafiki wenu katika usahihi pasipo
unafiki.(uwazi ni kama kuwa uchi kwa huyo rafiki)
Japo ni mtihani mkubwa
kutambua ukweli kuhusu mambo anayokwambia hivyo usiwe mwepesi wa kuamini mpaka
pale moyo utakapo jiridhisha.
V.anayekubaliane kuonyana
Kila mtu awe na uhuru
wa kumuonya mwezake kwa upendo, na kila mtu awe tayari kumsikiliza mwenzake kwa
kile anacho mwambia.
Pamoja na hayo usiwe
mwepesi katika kuchukua maamuzi jaribu kutulia na kwa upendo ulio nao na rafiki
unaweza kitu kilicho bora zaidi ambacho kitafanya urafiki ukawa wa maana sana.
Katika tofauti zenu na
namna mnavyo zimaliza hapo panaudhihirisho wa ubora wa urafiki na kumaanisha
kwenu.
Hasitokee mtu ajione
mwenye haki kuliko mwezake kwakua wote mnakamilishana katika kuleta maendeleo
yenu.
Msikilizane namuonane
kuwa wote mnahitajiana katika kutegemeana kwa ajili ya kufanikisha yaliyo mbele
yenu.
Hapa ni sehemu muhimu sana kwakua inaonyesha kwa kiasi
mnaingiliana katika kutimiza lengo lenu, hii hatua isipo fanyika kwa ungalifu
inaweza leta madhara makubwa sana.
Hii hatua inakuwa na
shida sana kama tu hamjatambua misingi ya urafiki wenu na kuipa nafasi kwa
ajili ya kufikia mahali mlipo kusudia.
Mnapokuwa mkisaidiana
jua kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa vizuri kwa asili yake bali wote
wanatengenezwa kuwa vizuri wanao kubali basi wanakuwa vizuri.
Mashindano sio sehemu
yenu,japo kutakuwa na mpishano ila msiluhusu katika mabishano yenu yaendelee
huku mkiwa katika mausiano ya urafiki.
VI.mpenda maendeleo ya pamoja.
Rafiki mzuri lazima
athamini maendeleo yako na hauzunike katika matatizo ya wengi hii ni shida sana
kwa marafiki walio wengi katika kutekeleza swala zima.
Pindi utakapo muona mtu
anaelewa vizuri swala linalo kukabili halafu akawa na wewe kanakwamba aelewi
kinacho kukabili huyo si rafiki mzuri.
Kama kweli ni rafiki
mzuri huwa atapenda kuona furaha yake basi panakuwa na furaha yako ili wote
mfurahi pamoja.
Hakuna urafiki ulio
mzuri kama ukimuona mwenzako analia nawe ukalia pamoja nae ili siku nawe
utakapolia mlie wote.
Ni mtu katika mipango
yake mizuri uwa anakufikiria na wewe pia anakuhusisha pale inapo bidi.
Ni mtu anayejali kesho
yako iwe katika hali iliyo njema na usahihi ili kuleta katika ustawi ulio bora
nakufanikisha yale yaliyo magumu kwake.
Hali hii pia iwe ndani
yako na wala usiitegemee kuiona kwa mtu mwingine wakati wewe ndani kuna
ubinafsi kamwe kudumu katika huo utofauti wa namna hiyo.
Hii ni ishara kubwa
sana ya kutambua udhati wa urafiki wenu
nikutambua nafasi yako kwake vile anavyokutambua ndivyo atakuhusisha inje
ya hapo hawezi kukuhusisha.
Uwezi kujivunia huyu ni
rafiki mzuri kama tu ujaona kwa udhati namna anavyo husika na maisha yako kujua
unafanya nini sasa na unamatarajio gani na je! Utafikaje huko.
Urafiki sio kula pamoja
wala kulala pamoja, au kushirikiana katika nguo bali namna gani
unavyomuandalia/mfikiria kesho nzuri ndugu yako.
Japo unatakiwa kuwaza
vizuri kwa wote lakini rafiki lazima usimamie kuhakikisha kuahakikisha mnaenda
pamoja.
Ifike kipindi mtu mmoja
akipata na mwingine akikosa haina shida kwakua unajua akipata yeye basi umepata
wewe kama sivyo basi huo sio urafiki wa kweli.
VII.anayetambua/thamini udhaifu wako,
Rafiki wa kweli huwa
atumii udhaifu wako katika kukufanya uwe mnyonge bali usimama katika nafasi ya
kukutegemeza ili uweze kuimarika na uonekane wa maana sana.
Tambua unapotambua
udhaifu wa mtu aliye rafiki yako fanya kwa uzuri huku ukitambua nawe ni dhaifu
katika upande mwingine.
Unapo kuwa na rafiki
yako lazima utambue furaha yake ndio burudiko lako na sivinginevyo, ni vizuri
utambue anaye weka ni Mungu kwaiyo haina uhusiano na mtu kupenda au kuto penda.
Kama mtu athamini
udhaifu wako jua kwamba mtu huyo hana shirika la kweli na wewe kwa kuwa
unahitaji kuona namna anavyo onyesha upendo wake kwako.
Anayetambua kuona maana
ya wewe kuwa katika hali iliyo njema haone maana yaw ewe kuwa rafiki yako.
VIII.anayependa mshirikiane
Ni mtu anaye tambua
uthamani wa uwepo wako japo inawezekana kufanya hata akiwa peke yake kwakua
anatamani mfanikiwe kwa pamoja.
Pindi anapofanya
shughuli yoyote pamoja na wewe anaona kuna kutiana nguvu na kufanya shughuli
kwa ufanisi zaidi.
Mioyo yenu inatambuana
katika yote mnayo shirikiana katika kufanya jambo ambalo mnashirikiana.
Uwepo wa mmoja wapo
inakuwa chachu nzuri katika kufahamiana na kuonana katika utendaji wenu kwa
ufasaha zaidi.
Huwa hamshirikiani kwa
sababu mnatakiwa tu mshirikiane bali ni hali yenu ya ndani inakuwa na uhitaji
huo, utendaji wenu unatawaliwa na furaha.
Hana ubinafsi ndani
yake bali anafanya yote kwa moyo wa kupenda na huku akitambua kuwa wewe ndio
yeye kwaiyo kama nafsi yake ilivyo ndivyo anavyo ona fahari juu yako.
Prepared
by:
“Rafiki mzuri kwa hatua
bora ya maisha”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni