Alhamisi, 29 Agosti 2013

moyo ulio jeruhiwa



MOYO ULIO JERUHIWA
Moyo ni sehemu muhimu sana katika mwili wa binadamu, na jeraha lolote linaweza kuathiri maisha yako kwa kiwango fulani mathalani mtu anapo vunjika mguu au kujeruhiwa hakika ilo jeraha litaweza kumfanya kushindwa kufanya jambo fulani kwa muda fulani halafu baadae hali ikarudi kuwa hali ya kawaida vilevile hali hii inaweza kutokea ikaathiri sehemu yoyote katika mwili, lakini sio jeraha la moyo hili ni jeraha ambalo kutibika kwake uwa linahitaji uangalifu wa hali ya juu sana.
Kitu kikubwa kinacho fanya majeraha katika moyo ni MAUSIANO. Tuangalie kwa namna ipi mausiano yanaleta majeraha katika moyo kwa kuangalia aina ya mausiano.

Mausiano kazini!
Hii ni sehemu moja ambayo moyo unaweza kujeruhiwa na kusababisha maumivu katika moyo  kwa kiwango kikubwa inaleta huzuni na hata magonjwa kuzidi kushamili katika miili yetu.
Vipo vikwazo ambavyo vinakuwa vinatokea kazini inaweza kuwa miongoni mwa wafanya kazi wezako au bosi wako.
Na tatizo kubwa linakuwa pale tu kila mtu anapotaka kutimiza maslahi binafsi na pindi anapokosa anaweza fanya jambo ambalo likaleta pigo kwa mwingine.
Ni wazi kuwa pindi moyo wako unapo jeruhiwa basi utendaji wako unashuka na ufanisi kupungua.
Sio jambo ambalo mtu analitegemea kuwa litatokea bali pindi litakapo tokea linaleta mvurugiko katika maisha yake kwa ujumla wake.
Pindi unajeruhiwa kazini katika Nyanja ya kimapenzi (hali ya kutaka kushirikiana kimapenzi pasipo ridha ya mtu binafsi) na Nyanja ya kutofurahia mafanikio yako hivyo upelekea kufanya uchochezi wa wewe kufukuzwa kazi au kufanya kazi katika mazingira.
Wako watu wanafanya kazi katika moyo ulio jeruhiwa wanavumilia tu, kwa sababu utaishije! Na hili uishi unahitaji hela hivyo unahitaji kazi ambayo itakuwezesha kupata fedha kujikim kimaisha na watu waliokaribu yako wanahitaji msaada wako. Mtu katika hatua hii anawaza mengi kuacha kazi, kubadilisha kazi na mengine mengi.

Mausiano ya kimapenzi!
Hili ni jambo ambalo limesababisha maumivu mengi katika jamii hii ya leo, sio kitu cha kushangaza mtu kubadilisha mausiano ya kimapenzi mara nyingi katika kipindi kifupi sana.
Kama pange kuwa na hospitali ya majeraha yanayo sababishwa na mausiano ya kimapenzi hospitali zinge jaa sana na hata kukosa nafasi ya kuwaweka wengine.
Ki ukweli mtu anapoingia katika mausiano haya mazuri matamu zaidi ya asali na chochote kinachofanana na hayo anatumaini kusonga mbele na kuishi ambayo yalikuwa ndoto yake tangu alipo kuwa kijana mdogo.
Majeraha haya yamepelekea watu kusema sihitaji kusikia mwanaume akinitongoza, na kamwe sitatumia muda wangu kufikiri kuhusu mwanaume/wanamke na wengine hata kujiua.
Majeraha yanayotokana na mvunjiko wa mausiano haya yamekuwa yakiongezeka siku baada ya siku kadili dunia inavyoenda ndivyo majeha haya yanazidi kuchukua nafasi katika sura mbalimbali, na kupelekea imani ya watu kukosa kuamini kama kuna mapenzi ya kweli zaidi ya pesa na muonekano mzuri wa mtu.

Sababu kubwa na mchafuko wa mausiano ya namna hii ni kutoishi maisha yenu bali ya watu wengine! Ambao hamuwajui, hivi sasa mausiana haya yamekuwa ni maonyesho (fasion), sanaa na mashindano na hata kujilinganisha (wivu pasipo akili).
Haya mausiano yamejenga historia katika maisha yao ambayo hawawezi kusahau bali imebaki jeraha ndani ya maisha yao.

Hali hii iepelekea kupoteza maana ya ndoa, wamefanya kuwa ni jambo ambalo la kuangaliana baadae kila mtu aendelee na mambo yake lakini sio jambo ambalo Mungu amelikusudia.
Napia watu wengi wanaingia katika ndoa sio kwa ridhaa yao wenyewe bali kwa shinikizo la wazazi, ndugu, jamii au rafiki.
Na hata kuchukiana pasipo kuangaliana mpate kuchukua uamuzi wa busara. Na hali hii sio kwa ndoa ambazo zinachipukia bali hata kwa wale waliotayari katika ndoa pamekuwa na shida kubwa sana! Kwa maana nyingine ulimwengu huu wa wapendanao umechafuka sijui utarudi katika hali hile ya awali.
Sasa hivi sio ajabu baba kufanya mapenzi na mwanae, mama kufanya mapenzi na mototo wake na hata watu wenye umri mkubwa kutembea na watoto wenye rika moja na wajukuu zao.

Mapenzi yamekuwa pesa, mfumo wa mapezi tulio nao hauna mfano hatutofautishi uchumba na ndoa kila mtu anafanya kwa namna anavyoona yeye ajali usahihi wa jambo hilo.

Kiukweli ndoa imepoteza thamaniyake japo mbwembwe zimeongezeka Sana hasa katika sherehe za harusi. Sasa hivi ndoa ni kukubali mateso, maumivu kutengwa na kufanyiwa jambo ambalo linapoteza utu wako na linaathiri maisha yako kwa ujumla.
Ndoa zimeongeza gharama na sio kuongeza upendo!!!!!!!!!!

Ki ukweli misingi ya mausiano ya kimapenzi haipo hivyo imekuwa rahisi kuvunjika kwakua hakuna nguzo za kushirikilia hazipo.
Watu wameona vyema wajifanyie mapenzi wenyewe kuliko kuolewa au kujiingiza katika mausiano ya kimapenzi.
Ni wazi usipoelewa misingi ya ndoa na kuifuata kamwe hauwezi ukawa na ndoa imara kwani hii iko wazi sana kile unacho kipanda ndicho utakacho vuna, usipande bangi ukategemea kuvuna mchicha!!!



Mausiano ya kijamii!!
Mbali na mausiano hayo yalitangulia pia moyo uweza kuumizwa kutokana na mausiano ya jamii inayokuzunguka.
Jirani yako anakuonaje wewe binafsi unawaza nini juu yako na kweli anawaza mazuri juu yako au yuko na kujitanguliza binafsi.
Jamii inahusisha na watu wa karibu pamoja na wazazi wako na wale unaoshirikiana (rafiki) ni kwa namna ipi mitazamo yao na vitendo vyao vinavyo asili maisha yako.
Namna wanavyo tumia mawazo yao kutawala utashi wako ambayo yamejengwa katika misingi yao binafsi yanayo nyima uhuru wako katika kufikia hatma ya maisha yako. Japo sio kila mawazo wanayokupa usiyape nafasi ndani yako.
Majeraha ya moyo ya nakuja pale tu wanapo vunja ndoto yako nzuri na kukupa ndoto yao ambayo ni kinyume cha utashi wako na hata kupelekea maumivu ndani ya maisha yako na kutoona umuhimu wao kwako.
Katika jamii inayo kuzunguka namna wanavyo changia katika kuhakikisha kurudisha nyuma maendeleo binafsi maneno ya kukuvunja moyo, kujaribu kurudisha nyuma maendeleo yako kuweka vikwazo vile ambavyo unapigana kutoka pale ulipo.
Ndani ya jamii unaweza kufanyiwa vitendo ambavyo vita athiri maisha yako kisakolojia na kimwili mathalani kubakwa, kuvamiwa na kuathiri mwili wako na kuchukuliwa mali zako na hivyo kurudisha nyuma maendeleo binafsi.
Namna jamii inavyo kutendea jua ndivyo wanavyo jeruhi moyo wako hivyo kuendelea kuvumilia na kuendelea kuangamia.


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

Tufanye nini………wakati ujao!!!!!!!!!!!!!!!!!

Alhamisi, 22 Agosti 2013

RAFIKI NI NANI?



RAFIKI NI NANI?

Rafiki ni mtu wa muhimu sana,kwakua katika kuwa nae unapata kujua upande mwingine wa maisha yaani nini  huyu rafiki yako amepitia katika mwenendo mzima wa maisha yake na nini anajua kuhusu maisha kwa ujumla wake(mtazamo wake kuhusu maisha) kwakua pasipo yeye kukutana na wewe usinge ya jua, vilevile katika kukutana/kuwa na rafiki unaweza kubadili kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine(mchango wake katika kuyainua maisha yako kimawazo au uchumi)
Ni kawaida rafiki mzuri watu hudumu nae nautamani kuishi nae wakati wote na rafiki asiye mzuri watu uvunja husiano wao,kwakua hukosa kuona umaana wa kuwa na rafiki pasipo kuona mchango mzuri  katika maisha yake.

Hivi ni rahisi kutambua huyu ni rafiki mzuri au rafiki mbaya kwakusikia habari zake au kwa kumuona kwa kipindi kifupi?
Rafiki ni mtu muhimu sana kwakua wako watu  waliotoka kimaisha kutokana na msaada wa rafiki na wako watu ambao hawajatoka kimaisha kutokana kutokana kukosa rafiki au kukosa rafiki ambaye anayeweza kumtoa mahali alipo na kwenda sehemu nzuri.
Sikuzote matarajio ya rafiki ni kuwa nae wakati wote akusitiri katika aibu yako na akukosoe katika pale unapoenda vibaya na rafiki wa namna hii ndipo utaona umaana wa kujivunia urafiki wenu,
Ninapozungumzia rafiki inawezekana kuwa wa jinsia yoyote wa kike au wakiume ili mradi anatimiza wajibu wake kama rafiki.(rafiki ni rafiki jinsia sio jambo la kulipa kipaumbele kwa kuwa alina maana unachohitaji ni kupata mtu ambaye anatambua nafasi yake kwako.
Katika dunia tuliyonayo wako watu ambao wameinuka kutoka na usaidizi rafiki walio karibu sio nyanja moja bali sehemu yote ya maisha binafsi.
                                                               Rafiki wa karibu!
Mtu naweza kuwa na rafiki aliye mbali na aliye karibu (mtu ambaye mnaonana mara kwa mara) na kushirikiana katika mambo mnayo yakabili pamoja.
Mtu ambaye athri yake inawezekana kuonekana kwa haraka ni Yule aliye karibu yako kwakua jambo atakalofanya litakuwa udhihirisho mkubwa.
Lakini kumbuka kuwa sio wote unao wapenda wanafaa kuwa marafiki zako, kwakua kunatofauti kubwa kati ya watu unao wafahamu na watu ambao ni marafiki zako. Japo wote unaweza kuwashirikisha lakini yako kuna kitu unategemea akifanye ili arudishe matumaini ndani ya moyo wako.
Vile rafiki yako alivyo ndivyo atakavyo weka namna yako utakavyo onekana endapo tu kama utamkubali ndani ya maisha yako, kwakua unaweza kuwa na mtu aliye karibu sana na wewe na hata mkashirikiana mambo mbalimbali hata ya mwilini lakini usimpe nafasi ndani yako na wala asi athiri maisha yako.
Iwakorintho 15:33
Ni hatari sana kuwa narafiki ambaye hakusaidii kukupeleka katika njia ambayo Mungu anataka uende.(udhihirisho wa urafiki wa kweli haupo katika kusema tu bali ni mchango unao onekana ndani ya maisha yako)
II nyakati 22:4-5
Mathayo 16:26
Rafiki asiye jua apasalo kufanya kwako huyo ni sumu sana kwakua kwakua anaweza kukupeleka kusiko kusaidia lakini kwa rafiki anayetambua wajibu wake kwako yeye anaye weza kurudisha furaha mahali pasipo na furaha na matumaini pasipo matumaini, kicheko pasipo kicheko na hata kuondoa upweke na simanzi ndani yako.
Ni wazi rafiki mzuri ili afanye mazuri juu yako kwanza hauna budi kumtambua halafu ukampa nafasi, pindi unapokosa kumtambua halafu ukampa nafasi ndani yako anaweza fanya jambo ambalo litaweka historia katika maisha yako.
Ili mwende pamoja lazima muwe zaidi ya kuwa pamoja yaani muwe na nia moja katika kukubaliana yale mtakayofanya katika moyo ulio safi.
Kamwe rafiki yeyote ambaye amjaambatana katika kunia mamoja ni vizuri kuachana nae kwakua uwezi kumsaidia kwa kumvumilia/kwa kuvuta subira atakuharibia au kukuchelewesha.
Lazima upate rafiki ambaye mtazungumza mambo ambayo yatapata kibali kwa Mungu katika maendeleo yenu binafsi na hatma njema iliyojaa Mungu mbali na hapo utapotea hakuna mapumziko.
Mithali 14:12

                                           Sifa za rafiki aliye bora:
Kumbuka kila rafiki ambaye unae anao mchango katika kukutengeneza au kukuharibu jambo hili lazima ulichukulie katika uzito wake.
Maandiko ya mungu yanasema,
“ndege wanaofanana ndio wanao ruka pamoja….”
Asikudanye mtu siku zote kile unacho kisikia, kukiona na kikipata nafasi ndani yako kinafanyika sehemu ndani ya maisha yako.
Kama unataka kuwa mtu wa maana lazima uwe na rafiki ambae ni wa maana vile rafiki yako alivyo ndivyo atakavyotoa mchango wake.

                                            I .awe anamjua Mungu.
Tambua kile alichonacho rafiki yako ndicho atachokupa sio kitu kingine ambacho hana, ni vizuri maisha yaonyeshe kweli anamuhofu Mungu,
Sio rafiki kila jambo yeye ni shabiki tu ajali jambo hili lina mpendeza Mungu au la! yeye ukulupikia maadam lina manufaa kwake.
Tambua sisi sote tumetoka kwa Mungu na kwa Mungu tutarudi, mambo ya dunia yanapita japo yanavutia ila angalia yasikutenge na Mungu kwakua Mungu yupo mahali pote na hata dumu milele.
Hivyo rafiki mzuri pamoja na mambo mengi ni mtu anayekukumbusha kuwa umetoka wapi?
“Watu wawili hawawezi kwenda pamoja isipokuwa wamepatana”
Hakikisha mwenendo mnatembea ni mwendo ulio na nuru ya Mungu ili mambo yenu Mungu hayafanikishe.

                                                II.anayejiheshim
Ni vizuri huyo rafiki lazima ajue maana ya heshima na anayejiheshim na anawaheshim watu wengine.
Tunapozungumzia hatuzungumzii ustahara wa kusalim (kupiga goti, sauti ya upole) ni zaidi hapo heshima ni namna unavyowaelewa watu na utu wao.
Anachokifanya ndicho hicho anachokimaanisha hana utofauti wa kauli ya mdomo na moyo wake.
Thamani ya watu kwake huwa haijengwi na kipato cha fedha, muonekano au maneno mazuri ambayo yanazungumzwa na mtu husika.
Ni mtu ambaye anawajali watu Kama anavyo mjali Mungu kwa kuwa watu tumetoka kwa Mungu kumpenda Mungu pasipo kuwapenda watu ni bure.
Luka 2:52
Japo wanadamu wote sio wema bali wewe fanya wema kasha uende usingoje matokeo.
Maandiko yanasema:
“Utampendaje Mungu usiye muona wakati unamchukua jirani yako……”
Katika dunia ni jambo la kawaida kumchukua binadamu wenzako halafu ukasema nampenda Mungu.(huwezi kuwapenda wazazi halafu ukawachukia watoto kwakua watoto ni sehemu ya wazazi)
Mathayo 5:43-48


                                                 III.kielelezo safi
Rafiki mzuri lazima mwenendo wake unakuwa mwelekeo mzuri na sio lazima awe kiongozi wa jamii,japo anaweza kuwa kiongozi wake binafsi.
Ni mtu ambaye anajua iko jamii wanahitaji kujifunza kupitia yeye inategemea na rika alilonalo
Kielelezo safi ni kitu muhimu sana kwakua atakuachia mambo ya mazuri ambayo utayatumia kaika maisha yako.
Ni kweli unaweza kuwa na watu wengi wasiwe kielelezo kwako lakini asiwe rafiki kwakua ana nguvu ya kukushusha au kukuimarisha.
Lazima kielezo safi ziwe sifa ambazo binafsi anazizingatia kwa mwenendo mzima wa maisha yake binafsi.
Mathayo 5:16
Japo kuna watu wenye maadili mema lakini pamoja na hayo unahitaji kuwa na Mungu ili akuwezeshe kudumu katika kielelezo safi kwani katika dunia ya sasa unaweza kukutana jamii wakabadilisha ule mfumo wako wa maisha kwa ujumla wake.
Hakikisha awe anaongea mambo ambayo yanajenga yaliyo na mufaa kwa jamii inayo mzunguka, sio mtu aliye jaa majungu na visasi ndani yake,
                                                    IV.mwazi,mkweli
Lazima anapokuwa na wewe ni mahali ambapo moyo wake unakuwa na nguvu na kusonga mbele kwa hali hiyo ni lazima awe mwazi kwako( hali ya kweli itoke ndani yake aseme kanakwamba anajiambia mwenyewe)
Hii ni moja ya nguzo ya kweli katika maisha  yenu kama hamna hali hii jua kwamba urafiki wenu unauhalakini au dosari au kutoaminiana.
Lazima muonane ninyi ni zaidi ya kila kitu pindi mnapo kutana mnajenga vitu ambavyo vinakuwa na faida katika maisha yenu binafsi.
Kama rafiki ambaye sio muanzi jua huo urafiki wenu unadosari kuwa makini au jipange kwa lolote kutokea wakati wowote.
Uwazi ni ishara kubwa sasa mmeanza kuingiliana katika urafiki wenu katika usahihi pasipo unafiki.(uwazi ni kama kuwa uchi kwa huyo rafiki)
Japo ni mtihani mkubwa kutambua ukweli kuhusu mambo anayokwambia hivyo usiwe mwepesi wa kuamini mpaka pale moyo utakapo jiridhisha.

                                                  V.anayekubaliane kuonyana
Kila mtu awe na uhuru wa kumuonya mwezake kwa upendo, na kila mtu awe tayari kumsikiliza mwenzake kwa kile  anacho mwambia.
Pamoja na hayo usiwe mwepesi katika kuchukua maamuzi jaribu kutulia na kwa upendo ulio nao na rafiki unaweza kitu kilicho bora zaidi ambacho kitafanya urafiki ukawa wa maana sana.
Katika tofauti zenu na namna mnavyo zimaliza hapo panaudhihirisho wa ubora wa urafiki na kumaanisha kwenu.
Hasitokee mtu ajione mwenye haki kuliko mwezake kwakua wote mnakamilishana katika kuleta maendeleo yenu.
Msikilizane namuonane kuwa wote mnahitajiana katika kutegemeana kwa ajili ya kufanikisha yaliyo mbele yenu.
Hapa ni sehemu  muhimu sana kwakua inaonyesha kwa kiasi mnaingiliana katika kutimiza lengo lenu, hii hatua isipo fanyika kwa ungalifu inaweza leta madhara makubwa sana.
Hii hatua inakuwa na shida sana kama tu hamjatambua misingi ya urafiki wenu na kuipa nafasi kwa ajili ya kufikia mahali mlipo kusudia.
Mnapokuwa mkisaidiana jua kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa vizuri kwa asili yake bali wote wanatengenezwa kuwa vizuri wanao kubali basi wanakuwa vizuri.
Mashindano sio sehemu yenu,japo kutakuwa na mpishano ila msiluhusu katika mabishano yenu yaendelee huku mkiwa katika mausiano ya urafiki.

                                                VI.mpenda maendeleo ya pamoja.
Rafiki mzuri lazima athamini maendeleo yako na hauzunike katika matatizo ya wengi hii ni shida sana kwa marafiki walio wengi katika kutekeleza swala zima.
Pindi utakapo muona mtu anaelewa vizuri swala linalo kukabili halafu akawa na wewe kanakwamba aelewi kinacho kukabili huyo si rafiki mzuri.
Kama kweli ni rafiki mzuri huwa atapenda kuona furaha yake basi panakuwa na furaha yako ili wote mfurahi pamoja.
Hakuna urafiki ulio mzuri kama ukimuona mwenzako analia nawe ukalia pamoja nae ili siku nawe utakapolia mlie wote.
Ni mtu katika mipango yake mizuri uwa anakufikiria na wewe pia anakuhusisha pale inapo bidi.
Ni mtu anayejali kesho yako iwe katika hali iliyo njema na usahihi ili kuleta katika ustawi ulio bora nakufanikisha yale yaliyo magumu kwake.
Hali hii pia iwe ndani yako na wala usiitegemee kuiona kwa mtu mwingine wakati wewe ndani kuna ubinafsi kamwe kudumu katika huo utofauti wa namna hiyo.
Hii ni ishara kubwa sana ya kutambua udhati wa urafiki wenu nikutambua nafasi yako kwake vile anavyokutambua ndivyo atakuhusisha inje ya hapo hawezi kukuhusisha.
Uwezi kujivunia huyu ni rafiki mzuri kama tu ujaona kwa udhati namna anavyo husika na maisha yako kujua unafanya nini sasa na unamatarajio gani na je! Utafikaje huko.
Urafiki sio kula pamoja wala kulala pamoja, au kushirikiana katika nguo bali namna gani unavyomuandalia/mfikiria kesho nzuri ndugu yako.
Japo unatakiwa kuwaza vizuri kwa wote lakini rafiki lazima usimamie kuhakikisha kuahakikisha mnaenda pamoja.
Ifike kipindi mtu mmoja akipata na mwingine akikosa haina shida kwakua unajua akipata yeye basi umepata wewe kama sivyo basi huo sio urafiki wa kweli.
                       
                                          VII.anayetambua/thamini udhaifu wako,
Rafiki wa kweli huwa atumii udhaifu wako katika kukufanya uwe mnyonge bali usimama katika nafasi ya kukutegemeza ili uweze kuimarika na uonekane wa maana sana.
Tambua unapotambua udhaifu wa mtu aliye rafiki yako fanya kwa uzuri huku ukitambua nawe ni dhaifu katika upande mwingine.
Unapo kuwa na rafiki yako lazima utambue furaha yake ndio burudiko lako na sivinginevyo, ni vizuri utambue anaye weka ni Mungu kwaiyo haina uhusiano na mtu kupenda au kuto penda.
Kama mtu athamini udhaifu wako jua kwamba mtu huyo hana shirika la kweli na wewe kwa kuwa unahitaji kuona namna anavyo onyesha upendo wake kwako.
Anayetambua kuona maana ya wewe kuwa katika hali iliyo njema haone maana yaw ewe kuwa rafiki yako.
                                             VIII.anayependa mshirikiane
Ni mtu anaye tambua uthamani wa uwepo wako japo inawezekana kufanya hata akiwa peke yake kwakua anatamani mfanikiwe kwa pamoja.
Pindi anapofanya shughuli yoyote pamoja na wewe anaona kuna kutiana nguvu na kufanya shughuli kwa ufanisi zaidi.
Mioyo yenu inatambuana katika yote mnayo shirikiana katika kufanya jambo ambalo mnashirikiana.
Uwepo wa mmoja wapo inakuwa chachu nzuri katika kufahamiana na kuonana katika utendaji wenu kwa ufasaha zaidi.
Huwa hamshirikiani kwa sababu mnatakiwa tu mshirikiane bali ni hali yenu ya ndani inakuwa na uhitaji huo, utendaji wenu unatawaliwa na furaha.
Hana ubinafsi ndani yake bali anafanya yote kwa moyo wa kupenda na huku akitambua kuwa wewe ndio yeye kwaiyo kama nafsi yake ilivyo ndivyo anavyo ona fahari juu yako.

Prepared by:
                    Cothey Nelson       -  0764 018 535 or Cotheyn@yahoo.com
                  
                    James Adili Katiti – 0713 398 042 or James.adili19@gmail.com
       
                 Rafiki mzuri kwa hatua bora ya maisha”

Jumatatu, 12 Agosti 2013

Ushauri juu ya Mahusiano(uchumba) na Ndoa: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA

Ushauri juu ya Mahusiano(uchumba) na Ndoa: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA:                                                           NDOA: Ni vizuri kutangulia kutambua nini maana ya ndoa kabla hujaingiza k...

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA



                                                          NDOA:

Ni vizuri kutangulia kutambua nini maana ya ndoa kabla hujaingiza katika jambo lenyewe kwakua  pindi utakapo tambua inakupa kujipanga vizuri.zipo maana mbalimbali zinazotolewa na mashirika,mila na desturi,kisheria kuhusu ndoa.kiukweli ndoa ndio chanzo cha familia,jamii na hatimae taifa kwa ujumla.hivyo ni muhimu sana kujifunza na kutoa kipaumbele kujua misingi mizuri ya ndoa ili kupata taifa bora, japo jamii ya sasa kunatatizo kubwa la ndoa nyingi kuvunjika na matatizo yake ni mengi mathalani watoto wa mitaani.
                           1st position JESUS

Mambo ya kuzingaatia;
I. sio kila mtu anayekuvutia anafaa kuwa mwenzi wako.
-sio kila kizuri kinachopita mbele yako kinafaa kuwa chako.

II .sio kila mtu aliyekidhi vigezo vyako anafaa kuwa mwenzi wako.                                              -tambua swala la ndoa alihitaji kubahatisha ni swala makini sana lililobeba ukamilisho na mwendelezo bora wa hatima yako.
-ukikosa hatua ya kwanza inaweza kukupelekea kukosea hatua nyingine.

III .sio kila mtu ili mradi ameokoka anafaa kuwa mwenzi wako.
-tambua wokovu ni swala la mtu na Mungu na wala sio la kutazama kwa macho ukatoa maamuzi.
-wako waliovaa sura ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu wa kali sana.
-sio wote wanaoingia kanisani na kutoka basi ameniokoka na anafaha kuwa mke/mme wako.
Ni kweli mtu asiyeokoka anaweza kuwa mwenzi wako lakini kwa special case ambayo anaijua Mungu isiyousishwa na mataminio ya kimwili(fedha,kiwango cha elimu au jinsi alivyo)

IV.sio kila mtu mwenye uwezo (akili,fedha,busara,hekima) anafaa kuwa mwenzi wako.
-Tambua unakwenda kuishi na mtu mwenyewe na tabia zake na wala sio fedha zake na mambo mengine aliyonayo.
Sio wakati wote mtu atakuwa na hekima na busara wakati wote tambua huyo ni binadamu aliye na tabia kamili za kibinadamu.

V.sio kila mwenye uwezo wa chini(kifedha,akili,hekima) anafaa kuwa mwenzi wako.
Tambua mtu sahihi uja kwa mtu sahihi katika Mungu maana yeye ndio anayejua.

VI.sio kila mtu anayejua mambo mengi anafaa kuwa mwenzi wako.
Tambua mtu na mambo yake ni vitu viwili tofauti, unaishi na mtu na wala sio mambo anayo yajua yale yote ni ubinafsi wake.
Kuoa/kuolewa sio sifa bali ni mpango kamili wa Mungu kwako.
Hauhitaji usianishwe sana na  matamanio ya kimwili kwani roho na mwili haviwezi kupatana milele.

VII.sio kila mtu aliyekusudia anafaa kuwa mwenzi wako.
Usitake kulipa jema kwa jema,kwani yeye aliye kusaidia ujui ana malengo gani? Yanalingana na wewe.
Ni vizuri kuonyesha shukrani kwa jambo alilo kutenda lakini zipo namna nyingi sio lazima uonyeshe  shukrani kwa kutaka kuwa mwenzi wako.
Tambua mambo haya hayahitaji haraka kwani yapo na hautapitwa na hatua hii maadam unaye Mungu anaye kukuwezesha.

VIII.sio kila mtu mwenye mvuto/kivutio cha watu wengi anafaa  kuwa mwenzi wako.
Watu wengi wanavyo muona anafaha sio Mungu anavyoweza kumuona anafaha kwako.

IX.sio kila mtu aliyesoma au hakusoma anafaa kuwa mwenzi wako.
Mtu apangiwi bali Mungu anaona kesho yako ndio anakuandalia kwa kupatia mtu sahihi akufahae sasa na hata baadae.

NDOA ni mchanganuo wa mambo mengi yaliyopitiliza na sio jambo moja au mawili ambayo watu uwaza (kustarehe,kucheka na kuburudika)
Ndoa haina ufundi au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine ikiwa inafasi ndani ya ndoa yenu.
Ni vizuri utambue nini hasa maana ya ndoa katika hali ya kiMungu.(kusudi la Mungu katika ndoa)
Hiko tafsiri ya ndoa kwa maana ya kidunia ukiichukua na ukaingiza katika utendaji ni vita viwili tofauti hakika vitapasuka maana havichangamani.
Ndoa si kwakua umetamani tu unaoa au kuolewaau namna ulivyo upanga kwa muda mrefu ndio maana unaoa/kuolewa lakini ndoa ina maana zaidi ya hapo.
Napenda utambue kuwa ndoa sio sifa /ufahari katika jamii ili watambue kuwa sasa wewe ni mtu uliyeoa au kuolewa.
                          Torati 10:20-21
Ni maisha ya wawili yanahitaji mshikamano wa hali ya juu kwani maisha haya yanagharama.
Pamoja na hayo iwe ni kweli Mungu anaweza kuwatengeneza sio mengine.
Hasi kudanganye mtu ndoa si kama wale wanavyoishi bali ni vile na mwenzio mtakavyoishi au mnavyoishi.
Kwani ndoa  nyingi ni tofauti katika ulka,mtazamo na hata matamanio tofauti.

Nini maana ya ndoa hasa?
Ndoa ni muungamaniko wa watu wawili wenye jinsia tofauti(mke na mme) usio na kipaumbele sana matamanio ya kimwili bali katika maisha yaliyo jaa furaha kwa jinsi mlivyo na yenye kibali kwa  Mungu.
    Mwanzo 2:5-25
Kwa maana hii ndoa ni furaha,faraja,kicheko,burudani,matumaini maana Mungu yupo pamoja na ninyi
Kwa hakika haya ni maisha ambayo hutamani yesu harudi mapema.
Kwani mateso mengine shetani uwatesa kwakua hawajui maana ya ndoa.
    Mithali 2:11
Ni kweli ndoa ni muhimu japo si lazima lakini usalama wa maisha yako yaliyo jaa furaha na amani na maono ya maisha ya baadae katika Mungu ni muhimu sana. 
                              I wakorintho 7:1-9(8-9)
Tambua ndoa imara ina tegemea misingi imara sana usitegemee ukaendelea vizuri wakati misingi sio imara.
Ushauri!!!!!!!!!!
Sio swala la kukulupikia japo ni jema
Kwakua,
Jambo sahihi uja kwa wakati sahihi na mtu sahihi.
Ni bora wakuone unachelewa lakini huko katika mpango sahihi wa Mungu kuliko wakuone unaendelea vizuri /unaenda na wakati huku Mungu yuko mbali nawe.
Ni vizuri utambue kuwa Mungu anakupenda na anakuwazia yaliyo mema na mpango mzuri na anatambua na anathamini hisia zako.
                       Yeremia 29:11



Prepared by:
                   Cothey Nelson          – 0764018535 or cotheyn@yahoo.com
                
                  James Adili Katiti       - 0713398042 or James.adili19@gmail.com



 “tunaWAtakia maisha mema katika mungu”